Na Mwandishi Wetu, Arusha
Timu ya wavulana ya ULIPO TUPO kutoka kanda ya ziwa imeibuka kidedea kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya timu ya SDK ya Kanda ya Mashariki katika mechi ya fainali ya mashindano ya kombe la Super Cup 2003 yanayoendeshwa na benki ya CRDB.
Kutokana na ushindi huo, timu ya ULIPO TUPO imezawadiwa kitita cha shilingi milioni 13 kombe na medali ya dhahabu katika michuano hiyo iliyokuwa ikifanyika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid, Arusha.
Tmu ya Albarakha kutokea kanda ya Magharibi ambayo tangu mashindano hayo yaanze ilionekana kuleta upinzani kidogo kwa timu zingine imeambulia nafasi ya tatu katika mashindano hayo.
Timu ya SDK ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli na kabla ya mapumziko timu ya ULIPO TUPO ilifanikiwa kusawazisha na timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare ya goli 1-1.
Timu ya Ulipo tupo, ilirejea kwa kasi kipindi Cha pili na iliwachukua dakika chache kuongeza goli la pili ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuibuka kidedea.
Kwa upande wa wanawake Kanda ya ziwa pia imeendeleza ubabe dhidi ya timu kutoka katika Kanda zingine ambapo timu ya netiboli ya ULIPO TUPO imeibuka kidedea kwa kuifunga timu ya netiboli ya POPOTE INATIKI kutoka kanda ya kati Dodoma .
Kutokana na ushindi huo, timu hiyo imezawadiwa kitita cha shilingi milioni 9,kombe na medali ya dhahabu huku mshindi wa pili timu ya POPOTE INATIKI STD kutoka Kanda ya Mashariki ikizawadiwa shilingi milioni sita medali ya fedha na kombe na timu ya STD ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu na kuambulia zawadi ya kitita Cha shilingi milioni 4.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amewapongeza CRDB kwa ubunifu huo ambao amesema umeendelea kuongeza morali na kuibua vipaji kwa watumishi .
Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema mashindano hayo yana lengo la kujenga umoja na mshikamano kwa watumishi wa CRDB Nchi nzima.
Mashindano hayo yanahitimisha msimu wa tatu wa CRDB Super cup ambapo zilianza timu 12 za mpira wa miguu na timu 8 za netiball katika mashndano yaliyofunguliwa mwezi Agosti jijini Dar es salaam Agost 8 mwaka hu