Trump apandwa na hasira baada ya waandamanaji kuuvamia ubalozi wa marekani nchini iraq na kutaka kuuchoma moto

Rais
Donald Trump wa Marekani ameonyesha kuchukizwa na  maandamano makubwa
mbele ya ubalozi wa nchi hiyo huko Baghdad, mji mkuu wa Iraq lakini hata
hivyo akaishia kusema anaamini 
Iraq itatumia vikosi vyake vya usalama kuulinda ubaloz huo wa Marekani


Kauli hiyo ameitoa wakati ambapo anailaumu Iran kwa kuchochea vurugu hizo dhidi ya eneo lake. 

Wananchi
wa Iraq ambao ni wafuasi wa wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran
waliandamana kwenye ubalozi wa Marekani siku ya Jumanne huku wakiimba
nyimbo zinazosema ”Kifo cha Marekani,” wakirusha mawe, wakivunja
kamera za usalama pamoja na kulichoma moto eneo la mapokezi, wakilaani
mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani.


Mashambulizi hayo yaliyofanyika Jumapili iliyopita yaliwaua wapiganaji wapatao 25 wa kundi la wanamgambo wa Kataeb Hezbollah. 

”Tunatarajia
Iraq itavitumia vikosi vyake kuulinda ubalozi na tumearifiwa hivyo,”
ameandika Trump katika ukurasa wake wa Twitter. Trump amesema Iran
itawajibika kikamilifu kwa machafuko hayo.


Mashambulizi
ya Marekani yalikuwa ni kujibu shambulizi la roketi lililofanywa wiki
iliyopita na kumuua mkandarasi mmoja wa Kimarekani katika kituo cha
jeshi la Iraq, ambalo ni la karibuni kufnayika lililenga maslahi ya
Marekani nchini Iraq. 

Hakuna
kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini vikosi vya
usalama vya Marekani vimelishutumu kundi la Kataeb Hezbollah.

 

Trump amesema Marekani imejibu vikali shambulizi ambalo limemuua mkandarasi huyo na skwamba siku zote itafanya hivyo. 

Uhusiano
kati ya Marekani na Iran umekuwa ukizorota tangu Marekani ilivyojiondoa
kwenye mkataba wa kihistoria wa nyuklia wa Iran mwaka 2018 na kuweka
vikwazo vipya.


Hii
ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kadhaa kwa waandamanaji
kufanikiwa kuufikia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, uliopo kwenye
eneo lenye ulinzi mkali maarufu kama Green Zone. 

Vikosi
vya usalama ndani ya ubalozi huo walifyatua mabomu ya kutoa machozi
kuwatawanya waandamanaji nje ya ubalozi huo. Imeripotiwa kuwa zaidi ya
watu 20,000 walikusanyika nje ya ubalozi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *