Tulia trust yakabidhi msaada wa ndoo za maji kujikinga na corona

Na Esther Macha, Mbeya

Taasisi ya Tulia Trust imekabidhi ndoo arobaini na gallon thelathini na sita kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Jiji la Mbeya kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa corona.

Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa Tulia Trust Jacqueline Boaz alisema lengo la Taasisi hiyo ni kuinga mkono serikali katika mapambano dhidi ya corona.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Jiji la Mbeya Afrey Nsomba pamoja na kushukuru alisema vifaa hivyo vitasambazwa katika ofisi zote za Chama Jijini Mbeya.

Nao baadhi ya wanachama akiwemo Charles Mwaipopo na Venance Matinya walisema vifaa hivyo vitasaidia mapambano dhidi ya corona na kwamba vimekuja kwa wakati.

Kutolewa kwa vifaa hivyo kutasaidia mapambano dhidi ya corona kuanzia ngazi za mitaa na Kata kwa ujumla.

Mwisho.