Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (costech) yatoa mafunzo kwa waandishi wa habari na watafiti wa kanda ya masharikiKaimu Mkurugenzi wa TALIRI Dkt. Zabron akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari za Sayansi pamoja na watafiti wa kanda ya mashariki yanayofanyika Tanga

Afisa Utafiti Mkuu-COSTECH Dkt. Bakari Msangi akiwasilisha mada yake kuhusu Utafiti na umuhimu wa kusambaza matokeo ya Utafiti.

Washiriki wakifuatilia mada zinazowasilishwa.

Washiriki wakiendelea kupata mafunzo

Afisa programu ya mafunzo hayo kutoka COSTECH Bw.Method Rutechura akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo.
***
Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) imewakutanisha kwenye mafunzo waandishi wa habari na watafiti kutoka kanda ya mashariki ili kuwajengea uwezo wa kufikisha matokeo ya Sayansi teknolojia na ubunifu kwa walengwa.


Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo ya siku mbili kaimu Mkurugenzi idara ya Menejimenti ya taarifa Emmanuel Nnko aliyemwakilisha mkurugenzi mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu, amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa jitihada za Tume za kuhakikisha Tafiti zinazofanywa nchini ili ziweze kuleta tija kwa jamii.


Akifungua mafunzo hayo yaliyohusisha watafiti na waandishi kutoka kanda ya mashariki Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi za utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) Dkt. Zabron Nziku amesema Matokeo ya utafiti ndiyo yanayoweza kusaidia Uchumi wa viwanda endapo yatawafikia walengwa na kuyatumia.


Amesema kuwa tafiti nyingi zinafanywa lakini zinaishia kwenye vituo vya utafiti na hivyo wananchi na wadau wa tafiti hizo kutonufaika nazo wakati zimetumia fedha nyingi.


Amepongeza programu hiyo ambayo inafanywa na COSTECH nchi nzima na kuwataka waandishi wa habari kuyafanyia kazi ili yaweze kusaidia jamii ya Watanzania.


Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo Emmanuel Nnko ambaye ni kaimu mkurugenzi wa Idara ya menejimenti ya Maarifa kutoka COSTECH aliyemuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa Tume amesema mafunzo hayo ni muhimu kwani yanasaidia kuwaleta pamoja wansayansi na waandishi wa habari na kupanga mikakati ya namna wanavyoweza kushirikiana katika kusaidia jamii na Taifa kwa kubuni njia bora za kuwafikishia wadau matokeo ya tafiti hizo.


Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mafunzo kwa waandishi wa habari na watafiti ambayo yanafanyika nchi nzima ili kusaidia kufikia malengo ya kupata taarifa za tafiti mbalimbali zinazofanyika nchi nzima kwenye vituo na taasisi za Utafiti.


Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo Afisa programu ya mafunzo hayo kutoka COSTECH bwana Merchades Rutechura amesema ni kupunguza gepu kati ya watafiti na watumiaji wa tafiti hizo nchini.


Amesema kuwa toka mafunzo hayo yaanze kwenye kanda mbalimbali kumekuwa na ongezeko kubwa la Makala,vipindi na habari za Sayansi,teknolojia na Ubunifu na hivyo kusaidia jamii kujua ni wapi wanaweza kuzipata ili kuzitumia kwenye shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kuongeza tija.


Amewataka waandishi hao wa kanda ya mashariki inayojumuisha Mikoa ya Dar es salaam,Pwani, Morogoro na Tanga kutumia kusanyiko hilo kujua miiko ya utoaji wa taarifa na kujenga mashirikiano na watafiti ili kuweza kuwatumia katika uandaaji wa vipindi vyao.


Akiwasilisha mada kuhusu Utafiti na umuhimu wa kutoa matokeo ya utafiti Afisa Utafiti Mkuu kiongozi anayeshughulikia Makala na Machapisho kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi waandishi wa habari wana umuhimu Mkubwa katika kufanya kazi hiyo kwakuwa wanasikilizwa na kuaminiwa na jamii.


Dkt. Msangi amesema katika kazi yoyote kuna miiko na maadili yake hivyo waandishi wa habari nao ni lazima wajue miiko na maadili ya kuandika habari na kuandaa vipindi vya Kisayansi na ubunifu ili waweze kufanya kazi hiyo vizuri kwa maslahi ya taifa bila kuleta matatizo kwa mtafiti na mwandishi mwenyewe.


Amesema habari za kisayansi zinahitaji ubunifu kwenye kupeleka kwa walengwa kwa kuandika habari zenye lugha nyepesi, ufupi na kwa kutumia njia ambayo inaweza kuwafikia walengwa katika eneo fulani iwe redio,Televisheni au magazeti.


Dkt. Msangi amesema kuwa mbali na kuwafikia wakulima na wafugaji lakini pia inasaidia kuwafikia watoa maamuzi kutumia