Vijana watakiwa kuondokana na fikra mgando

Na Matukio Daima APP 

IMEELEZWA kuwa tatizo la kubwa   la  baadhi ya  vijana  toka  familia  zenye  mazingira  magumu  kutojikita  kuanzisha  miradi ya kiuchumi  ni  kutokana na  kujinyanyapaa  wenyewe  na  kuwa na fikra  mgando  za  kukata taamaa kama hawawezi  kufanikiwa  kiuchumi  hata kama  wakiwezeshwa .

Akizungumza jana katika  ukumbi  wa  Yatima  kijiji  cha  Igoda  kata  ya  Luhunga wilaya  ya  Mufindi mkoani  Iringa  mara  baada ya  mafunzo ya  mtazamo na  miradi ya  kilimo na  ufugaji  yanayotolewa  na taasisi  isiyo ya  kiserikali ya  R – LABS Tanzania  kwa  vijana  wa  mradi  wa  Youth Agency  Mufindi (YAM) meneja  msaidizi  wa  mradi  huo Danoford Mkumba alisema  changamoto ya  vijana  waliowengi  ni  kutawaliwa na  fikra  mgando  katika maisha yao  hivyo ni  vigumu  kufanikiwa katika maisha .

Mkumba  alisema  vijana  wanayo fursa   kubwa sana na  kufanikiwa  katika maisha  kutokana na  jitihada  kubwa  zinazofanywa na mradi huo  wa  YAM  pamoja  na serikali   kupitia  Halmashauri  zote nchini  ambazo  zimekuwa  zikitenga  fedha  kwa  ajili ya mikopo isiyo na  riba kwa  kundi  hilo la  vijana ,wanawake na  watu  wenye  ulemavu .

Alisema  kuwa  katika  mafunzo hayo  ambayo  yamelenga  kuwafundisha  fikra  inayokuwa na  fikra  mgando  yatasaidia   sana  vijana  hao  kujitambua  na  kuondokana na  fikra mgando na  kujikita  katika  fikra  inayokuwa  ambayo itawawezesha   kusonga  mbele   kimaisha  kwa  kuja  kuwa  na miradi ya  kiuchumi   kupitia raslimali zinazowazunguka.

Mkumba  alisema  baadhi ya  vijana  wanaamini  kuwa  wakitoka katika familia  duni  kwao ni vigumu  kufanikiwa  katika  maisha  ila  kwa  mafunzo hayo  vijana  hao  wataweza  kujitoa katika fikra  mgando na  kwenda  na  fikra  inayokuwa .

Washiriki  wa  mafunzo hayo Diana  Yohana  ,Saraphina   Tengelakwi  na Andason  Mpende wakielezea  faida ya  mafunzo hayo   walisema  wanamatumaini  makubwa ya  kuyatumia   kubadili  maisha  yao  kwa  kwenda  kubunia  na  kuendesha  miradi yao  ya  kiuchumi .

Diana  alisema  kwa  upande  wake  kutokana na ulemavu  wake  wa  ngozi  jamii  inayomzunguka    imekuwa  ikitoa  upendeleo mkubwa  kwake  na  shida ya  kutokuwa na mradi  wa  kufanya  ni  kutokana na kupata mimba  za  utotoni  hali  iliyopelekea  kukwamisha  ndoto yake ya  kusonga  mbele  kimaisha  hasa  katika masomo .

 Hivyo  alisema  kwa  mafunzo hayo ya  kuondokana na fikra  mgando  iliyokuwa  imemtawala  anaamini  wazi   kuwa  atakwenda   kuwa  mfano  mwema kwa  kuanzisha  mradi wake  ama  kutimiza  ndoto yake ya  kurudi  shule  kwenda  kusomea  ualimu  ili  kuja  kufundisha wenzake .

Huku  Saraphina  akidai kuwa   sababu  kubwa ya  vijana   kutokuwa na miradi yao ni  kutokana na  uwezo  wao  wa  kufikiri kimaendeleo na  wengi  wao  kuishia  kufikiri  kurudi  nyuma  kwa  kujitazama familia  wanazotoka  zilivyo duni na  wao  kukatishwa  tamaa ya  kusimamia  kufanya shughuli  za  kiuchumi na kwa mafunzo hayo wanaweza  kusimama  kusonga mbele zaidi .

Mradi  wa Youth Agency Mufindi (YAM)   umelenga    kuwawezesha  vijana  zaidi ya  770 wakiwemo  watoto  150 yatima  kutoka   kata   hizo tatu   ambazo  zote  zitaunganishwa na  vijiji  16  za  mradi  huo .

  mradi  huo wa  YAM ni wa miaka minne toka mwaka 2021/2024 umefadhiliwa na    serikali  ya Filands  chini ya taasisi yake ya Diaconess   kwa  ushirikiano  wa  serikali ya Tanzania chini ya Halmashauri ya  wilaya  ya Mufindi na taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation.      

MWISHO