Waahidi kusaidiana na serikali ujenzi miradi ya maendeleo

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wananchi katika kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wameahidi kuendelea kuiunga mkono serikali kwa kushirikiana kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo uwezeshaji wa huduma za afya kwenye kata hiyo.

Wameyasema hayo leo wakati wakiendelea na zoezi la kuchimba msingi kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Ihapa ambapo wameishukuru serikali kwa kutoa kiasi cha shillingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

Wamesema kuwa wapo tayari kujitoa kwa hali na mali pale wan apohitajika kushiriki katika maendeleo ya jamii hivyo wameiomba serikali iendelee kushirikiana nao ili kuweza kutatua changamoto ya ukosefu wa huduma ya afya kwenye kata hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko ambaye ameongoza zoezi hilo amewapongeza viongozi wa kata hiyo kwa kuhamasisha wananchi kuja kushiriki kwa pamoja katika shughuli hiyo  ambapo mwitikio ni mkubwa kwa wananchi hao

Akupeleka pendekezo kwa wakala wa barabara Mijini na Vijijini TARURA mkoa wa Shinyanga ili waboreshe miundombinu ya barabaraba kwenye eneo hilo ili kurahisha huduma ya usafiri katika utoaji wa huduma ya afya kwenye kituo hicho

“Nitazungumza na na wenzangu wa TARURA waweze kuimarisha barabara ili gari zpitike kwa uharaka na wananchi wapate huduma za afya vizuri”

Naye Diwani wa kata ya Old Shinyanga Enock Charles  amesema atasimamia kuhakikisha pesa zinazoletwa zinatumika kama zilivyoelekezwa ambapo amesema atakuwa mkali kwa mtu yeyoto atakae leta uvunjivu wa amani kwenye shughuli hiyo

Uzinduzi huo wa kuchimba msingi wameshiriki watumishi wa serikali, viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura pamoja na wakuu wa idara.