Wafanyakazi katika kampuni ya CRJE inayotengeneza mizani katika eneo la kata ya Kimokouwa wilayani Longido wakiwa wamejipanga tayari kwa kupewa Elimu namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU yaliyoandaliwa na Taasisi ya VUKA Initiative
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus akitoa elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi na kupima kwa hiyari kwa wafanyakazi wa kampuni ya CRJE katika maeneo ya kata ya Kimokouwa (w)Longido
Paulo Laizer Mtendaji wa Kata ya Kimokouwa akizungumza na wafanyakazi wa ujenzi wa barabarara katika eneo linakojengwa mizani wilayani Longido
Wafanyakazi katika kampuni ya CRJE inayotengeneza mizani katika eneo la kata ya Kimokouwa wilayani Longido wakiwa wamejipanga tayari kwa kupewa Elimu namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU yaliyoandaliwa na Taasisi ya VUKA Initiative
Wa kwanza kushoto Ni Mkurugenzi wa Taasisi ya VUKA Initiative bi Veronica Ignatus,akifuatiwa na Mkandarasi katika Kampuni ya China CRJE Hongchun Gao ,kutoka kulia ni Mratibu wa Ukimwi Mery Tairo (w) ya Longindo,wengine Mtendaji kata ya Kimokouwa Paulo Lazer na baadhi ya wafanyakazi kutoka Taasisi ya VUKA Initiative
Timu ya VUKA Initiative wakiwa katika Kata ya Kimokouwa eneo linalojengwa mizani .
Elimu ikiendelea kutolewa kwa wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi ya CRJE kwenye ujenzi wa mizani katika kata ya Kimokouwa (w)Longido
ZAIDI YA WAFANYAKAZI 250 WA KAMPUNI YA CRJE WAPATA ELIMU NAMNA YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Na.Mwandishi wetu Arusha
Imeelezwa kuwa Ukatili wa Kijinsia ni moja ya kisabaishi cha maambukizi ya virusi vya ukimwi hivyo jamii imeaswa kupiga vita kwa mikakati thabiti ili iweze kuwa salama,kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameshiriki katika kufikia lengo la Kimataifa la kuona maambukizi mapya ya ukimwi yanafikia 0% ikiwemo unyanyapaa,Pamoja na ubaguzi
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vuka Initiative Veronica Ignatus ambapo waliweza kutoa elimu kwa wafanyakazi 250 kutoka kampuni ya China CRJE katika kata ya Kimokouwa ambapo, aliweza kuwakumbusha kuwa bado UKIMWI upo katika jamii hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kupima kwa hiyari ili kuzifahamu afya zao
Bi Veronica alisema kuwa maeneo mengi ya mpakani kunakuwa na mwingiliano mkubwa wawatu hivyo jamii ikachukua tahadhari juu ya maambukizi na kuhakikisha kuwa hatua za kujilinda wao Pamoja na wapenzi wao.
Hivyo alitoa hamasa kwa wadau wote wa masuala ya UKIMWI,taasisi za dini ,taasisi za Umma,sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kuongeza ushirikiano katika shughuli za kudhibiti,ikiwemo kukemea matendo na tabia hatarishi ,kuelemisha jamii kubadili tabia na kufanya kampeni za kuzuia maambukizi mapya haswa kwa vijana wanaokua ili wakute taarifa sahihi juu ya UKIMWI
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa almashauri ya Longido Dkt.Jumaa Mhina Mratibu wa Ukimwi ha (w)Bi Mery Tairo alisema kuwa maeneo hayo ya Kimokouwa yana changamoto ,kutokana na mwingiliano wawatu na mahitaji ya kibiashara,hivyo jamii inatakiwa kuchukua tahadhari kwa kujali Afya zao
Tairo alisema mwingiliano huo unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya virusi vya ukimwi amesema wilaya hiyo inajitahidi kushirikiana na wadau ikiwemo VUKA INITIATIVE kutoa elimu kwa jamii ili ilweze kuchukua tahadhari.
Davies Assery Kweka ni Daktari bingwa wa magonjwa ya maambukizi kwa binadamu anasema kuwa, hofu ni chanzo kikubwa cha upotoshaji juu ya ukimwi kwani inasababishwa na ukosefu wa elimu sahihi
Assery alisema kuwa mtu anapochukua hatua ya kupima afya yake, akagundua kuwa anayo maambukizi ya virusi vya ukimwi,siyo mwisho wa kuishi kwani bado anayo nafasi kuendelea anaweza kuishi vyema kwa kufuata ushauri wawataalamu wa afya
Ametoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla waondokane na hofu kwani ukimwi unaweza kujikinga kam vile ambayo jamii inavyoshauriwa kutumia chandarua kwaajili ya kujikinga na malaria,kwani kinga bora ni tiba
MWISHO