Watendaji wa kuu wa Wakala wa Barabara kutoka nchi saba barani Afrika wametakiwa kuwa na mifumo sahihi ya taarifa za barabara itakayosaidia kuokoa fedha za Serikali ili kutambua mahitaji mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya barabara katika nchi zao kwa wakati unaofaa.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe katika mafunzo ya siku Saba yanayofanyika jijini Arusha amezitaka taasisi hizo kuja na majawabu sahihiyatakayoondoa changamoto kwenye Mtandao wa barabara katika nchi hizo.
Alisema kuwa pamoja na ujenzi ukarabati wa barabara zetu bado suala la takwimu za ujenzi na ukarabati hazijawekwa kwenye mifumo ya Kanzidata inaonyesha kutokuwepo hivyo kupoteza mapato ya serikali kwa
ucheleweshaji wa ujenzi kwa kukosa takwimu sahihi.
“Tanroads Tarura shirikianeni kwa pamoja katika kuanzisha kanzidata ya pamoja itakayosaidia kuweza kukarabati kujenga barabara zetu ndani ya
muda unaohitajika na kuondoa changamoto katika mfumo wa taarifa za barabara zetu za ndani kupata taarifa mapema na kuzitatua kabla hazijaharibika utasaidia kuokoa fedha za Serikali”
Kwa upande wake Katibu mtendaji wa Shirikisho la barabara nchini Hagai Bishanga Alieleza kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na wizara ya ujenzi na Uchukuzi na kuzishirikisha nchi 7 ambazo ni Msumbiji Tanzania Zimbabwe Siraleon Liberia Moroco Kenya na Uganda ili kupata uzoefu na kuja na maazimio ya pamoja yatakayopeleke ujenzi wa
barabara nzuri za kimataifa.
alisema kuwa bado kumeendelea kuwa na changamoto kubwa ya kukosa taarifa sahihi za mifumo ya ujenzi na ukarabati wa barabara zetu ili kuchochea uchumi wa mataifa yetu ikiwemo kutokuwa na takwimu sahihi
ambazo mifumo ya utambuzi na sera zisizokidhi mahitaji
Akizungumzia changamoto kubwa katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kuwa ni pamoja na fedha kidogo zinazotengwa ambazo hazikidhi mahitaji , mfano hapa nchini ni fedha inayotengwa ni nusu ya mahitaji
yaliokusudiwa.
Alisema changamoto nyingine Ni kutokuwa na mifumo sahihi inayotoa taarifa kuhusu matumizi ya barabara bila kuathiri matumizi ya barabara pamoja na sera zilizopo hazikidhi mahitaji.