Wahanga wa mafuriko 801 wapewa msaada na kampuni ya qwihaya

Waziri mkuu Kassim Majaliwa wa pili kushoto akiwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Qwihaya Leonard Mahenda wa kwanza kushoto alipotembelea kiwanda chake cha nguzo Maginga 
…………………………………..

 WANAHANGA  801 wa Mafuriko wakazi wa kitongoji  cha Mbingama  kijiji  cha Isele tarafa ya Pawaga wilaya  ya Iringa  wamepatiwa msaada wa zaidi ya shilingi Milioni 21.
 toka kampuni ya Qwihaya General Enterprises ya mkoani Iringa .mwandishi Francis Godwin anaripoti  kutoka Iringa 
Akizungumza kwa  niaba ya mkurugenzi wa kampuni  hiyo  meneja wa kampuni hiyo  ya Qwihaya General Enterprises  Leonard Mahenda ,meneja  wake  ambae alipeleka msaada   huo  kijijini kwa  wanahanga  Ntimbwa Mjema  alisema kwa kupitia sera yao ya kurudisha sehemu ya faida wanayopata kwa wananchi, kampuni yao imeguswa na tukio la mafuriko lilowakumba wananchi hao ili  nao  waweze  kuendelea  kuishi maisha ya furaha  zaidi .
“Baada ya kuwasiliana na mkuu wa wilaya na kuelezwa mahitaji ya wahanga hao, kampuni yetu kwa upande wake iliamua kutoa msaada wa roli tatu za nguzo hizi za ujenzi zenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 21 pamoja na mifuko 30 ya unga ya kilo 25 kila mmoja,” alisema.
Meneja   huyo  alisema kwa kupitia sera yao ya kurudisha sehemu ya faida yao kwa wananchi, kampuni yao itaendelea kutoa misaada ya aina hiyo na mingine muhimu kwa wananchi ili kuharakisha maendeleo yao mbali ya  kutoa msaada  huo   kwa  wahanga hao alisema wamekuwa  wakitoa misaada mbali mbali  pale  inapohitajika   kufanya  hivyo.
Wahanga wa  mafuriko hayo  mbali ya  kushukuru kwa msaada huo  mirunda kwa  ajili ya  ujenzi wa  nyumba zao za muda  bado waliomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia kupata bati kwa ajili ya kuezekea na vifaa vingine vitakavyowawezesha kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo za muda alisema John Msemwa kwa  niaba ya  wenzake .

Kuwa  wameridhia uamuzi wa serikali wa kuwahamisha moja kwa moja kutoka katika kitongoji chao kilichokumbwa na mafuriko hayo na kwamba watageuza eneo hilo kuwa sehemu ya mashamba yao ili kujiinua kiuchumi japo kutokana na kupoteza mali zote  uwezo wa kupata fedha za  kununua bati na kuanza makazi ya  kudumu kwa sasa ni mgumu  kwao .
Akizungumza kwa niaba ya ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Afisa Elimu Msingi Peter Fusi alisema pamoja na serikali kuendelea kushirikiana na wadau kurejesha katika hali ya kawaida maisha ya wahanga hao, tahadhari za kujikinga na janga la virusi vyacorona linatakiwa kuendelea kuzingatiwa.

Kuwa  msaada   huo  ni mkubwa  na serikali  ya wilaya  imefarijika  kuona  kampuni  hiyo ya  kizalendo  ikiwa ni kampuni ya kwanza  ndani ya  mkoa huo  kujitolea kwa  kiasi kikubwa  kuanza  kuwasaidia  wahanga hao wa mafuriko ambao wanahitaji misaada mbali mbali   kutokana na kukumbwa na janga kubwa ya mali  zao zote  kusombwa na mafuriko .

Aktoa pongezi hiyo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  katika tukio hilo la mafuriko  yalisababisha  kaya 218 zenye jumla ya  wananchi 801 kuachwa bila makazi  pia mali  zao zote kikiwemo chakula  chao cha akiba  ni miongoni mwa  vitu  vilivyo athiriwa na mafuriko hayo yaliyotokea mapema mwezi huu .

Aidha  alisema  msaada  huo  wa   mirunda kwa ajili ya  kujengea  nyumba  za muda za  kuishi wahanga hao wa mafuriko iliyotolewa na kampuni   hiyo ya Qwihaya General Enterprises itawawezesha wahanga hao waliohamishwa  toka katika kitongoji hicho kutumia msaada  huo  kujenga nyumba za muda wakati juhudi za ziada za serikali na wadau wake zikiendelea kufanyika  ili kuwawezesha kujenga nyumba za kudumu katika eneo jipya walilohamishiwa na  serikali ya  kijiji chao 
“Kitongoji kile ni eneo linalopitiwa na mkondo wa maji, na rekodi za nyuma zinaonesha wamekuwa wakisumbuliwa na mafuriko ya mara kwa mara pindi mvua za mfululizo zinaponyesha, kwahiyo serikali imefanya uamuzi wa kuwaondoa moja kwa moja, hawatakiwi kurudi tena,” alisema.
hata  hivyo  aliwaomba  wadau wengine   kuendelea  kujitokeza  kuungana na kampuni hiyo ya  Qwihaya General Enterprises  kujitolea kuwasaidia wahanga hao kurudi katika maisha yao ya kawaida  kwani  bado wanahitaji  misaada mbali mbali  mengi pamoja na ujenzi wa makazi mapya, wanahitaji pia msaada wa chakula, nguo na mahitaji mengine muhimu kuwawezesha kurudi katika maisha yao ya kawaida.

Mvua  kubwa  zinazoendelea  kunyesha katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Iringa na mikoa ya Njombe na Mbeya   imeendelea  kuleta madhara makubwa katika  tarafa ya Pawaga   jimbo la Isimani linaloongozwa  na  mbunge Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi ,Nyumba na maendeleo ya makazi kutokana na  eneo hilo  kuwa ni uwanda wa chini zaidi usio na milima   hivyo  maji  yamekuwa  yakijaa katika tarafa  hiyo  mithiri ya bwawa