Wajumbe cpa kanda ya afrika wakutana katika mkutano mkuu visiwani zanzibar


Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 50
wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Justin
Muturi akiongoza kikao cha Mkutano huo mbele ya Wajumbe wa Jumuiya hicho
katika hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Visiwani Zanzibar.
Kushoto kwake ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai na kulia
kwake ni Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndg. Stephen Kagaigai



Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge
Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Tawi la Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed
Said akichangia jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa 50 wa Chama cha Mabunge
ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, katika hoteli ya Madinat Al Bahr
Business and Spa Visiwani Zanzibar.



Wajumbe Chama cha Mabunge ya
Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika wakiwa  kwenye kikao cha Mkutano Mkuu
wa 50 wa Chama hicho katika hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa
Visiwani Zanzibar.


(PICHA NA OFISI YA BUNGE)