Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wameiomba serikali kuyaendeleza yale mazuri aliyoyafanya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa enzi za uhai wake ikiwemo kupinga ukabila na udini ili kulinda amani ya Taifa.
Wakizungumza na Redio Faraja katika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha baba wa Taifa hayati Mw.Julias Kambaeage Nyerere ambapo wamesema hayati Nyerere alipambana kuleta uhuru Tanzania bila kumwaga damu huku wakiwaomba viongozi wa serikali kuyaendeleza mazuri aliyoyaacha ili kulinda amani, upendo na utulivu katika nchi hii
Katika Kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha baba wa Taifa Mw. Julias Nyerere maadhimisho haya yameambatana na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru pamoja na wiki ya vijana kitaifa ambayo yote yamefanyika wilaya ya Chato mkoani Geita katika viwanja vya Magufuli mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameonya watu wanaojihusisha na kilimo cha bangi kwamba kinaathiri nguvu kazi ya taifa kutokana na baadhi ya vijana kutumia dawa hizo za kulevya.
Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kiuchumi kwa vijana ili kuwaepusha na vishawishi na kujihusisha na mataumizi ya madawa ya kulevya.
Maadhimisho hayo yamefanyika sambamba na kilele cha mbio maalumu za mwenge wa uhuru mwaka 2021 yanayokwenda na kauli mbiu inayosema “TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU, ITUMIWE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI”
Kama tunavyofahamu kila Ifikapo Tarehe 14 Oktoba Kitaifa huwa ni siku ya Kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mw. Julius Kambarage Nyerere aliyefariki
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa kiongozi wa Kitanzania alieiongoza Tanzania, na kabla ya hapo Tanganyika, kuanzia 1960 hadi alipostafu mwaka 1985. Anatambuliwa kuwa ndiye Baba wa Taifa.
Baba yake alikuwa Nyerere Burito (1860 -1942), chifu wa kabila la Wazanaki. Anafahamika zaidi kwa jina la Mwalimu – taaluma yake ya zamani kabla ya kujiunga na harakati za ukombozi. Nyerere alipata elimu yake katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda na pia katika chuo kikuu cha Edinburg cha Uingereza.
Alisaidia kuunda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), na Tanganyika ilipopewa serikali mwaka 1960, Nyerere alikuwa Waziri Kiongozi, na kuiongoza nchi hiyo kwenye uhuru wake mwaka mmoja baadaye, na kuwa waziri mkuu wa kwanza.
Tanganyika iligeuka na kuwa Jamhuri mwaka 1962 na Nyerere akawa rais wake wa kwanza pia. Mwaka 1964, Tanganyika iliungana kisiasa na Zanzibar na kuzaa Jahmhuri ya Tanzania, ambako Nyerere aliendelea kuwa rais hadi alipon’gantuka mwaka 1985. Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa na umri wa miaka 77.
Hayati Baba wa Taifa , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa Mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule ilikuwa Tanganyika
Kitaifa Maadhimisho hayo huambatana na sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mgeni rasmi atakuwa.
Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kuona mbali, Ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere anakumbukwa kwa Mambo mengi ya msingi aliyoyapa kipaumbele wakati wa uongozi wake
jambo mojawapo alilolisema julai 29/07/1985, kwamba “kazi iliyokuwa muhimu kuliko zote kwangu Mimi , ilikuwa ni kujenga Taifa lenye umoja kwa msingi wa heshima na usawa wa Binadamu.” Mwenyezi Mungu Mrehemu
Katika mafanikio makubwa ya Nyerere kwanza alijenga umoja wa Taifa kati ya watu wa makabila na dini, kulinda amani kwa muda mrefu iliyofanya Tanzania iitwe kisiwa cha amani pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na Lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa Taifa katika vita dhidi mvamizi Idi Amini wa Uganda
Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu akiwa bado anapendwa na wananchi wengi katika nchi
Hayati Julias Nyerere ni mmoja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama wilaya ya Musoma mkoa wa Mara, Tanzania wakati ule ni Tanganyika
Hizi ni baadhi ya nukuu za hayati mwalimu Julias Nyerere
Hatuwezi kuwa na matumaini ya kutatua matatizo yetu kwa kujifanya kuwa hayapo
Katika Tanganyika tunaamini kuwa ni waovu , watu wasiomuamini Mungu wanaoweza kuifanya rangi ya mwili ya binadamu kuwa kigezo cha kumpa haki zake za kiraia “. Akizungumza na Gavana wa Uingereza , General Richard Gordon Turnbull, kabla ya kuchukua kiti cha uwaziri mkuu mnamo mwaka 1960.
Hakuna taifa lenye haki ya kufanya maamuzi kwa ajili ya taifa jingine ; hakuna watu kwa ajili ya watu wengine. ( Kutoka ‘Ujumbe wa amani wa mwaka mpya ,Tanzania, Januari 1968).
“Umoja hautatufanya kuwa tajiri, lakini unaweza kuwezesha kuiepusha Afrika na watu wa Afrika kutoheshimiwa na kudhalilishwa “. Kutoka katika hotuba aliyoitoa Accra, Ghana, Machi 6, 1997
Watu wanapaswa kuhusishwa, ili kufikia maendeleo ya kweli. (Julius Kambarage Nyerere (1974)
Elimu sio njia ya kuepuka umaskini , ni njia ya kupigana nao.
“Demokrasi sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuiagiza. Demokrasi inapaswa kuendelezwa kulingana na nchi yenyewe “. Juni 1991 mjini Rio De Janeiro, Brazil.
Itakuwa yote ni makosa , na si jambo la muhimu , kuhisi kuwa lazima tusubiri hadi viongozi wafe ndio tuanze kuwakosoa ” Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.