Washiriki kutoka katika Bandari ya Tanga wakihudumia wateja katika banda lao |
Na Queen Lema, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amewataka vijana na watanzania wa mikoa ya jirani kutumia maonyesho ya tanz food 2022 ili kupata elimu na teknolojia za kujifunza fursa za kujiajiri.
Mongela ameyasema hayo wakati wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Kilimo ya Tanz food 2022 yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya magereza kisongo jijini Arusha.
Amesema kuwa kupitia maonyesho hayo ya siku tatu watanzania na vijana wanapaswa kuyatumia ili wajifunze mbinu na teknolojia za kilimo bora.
Kwa upande wake mratibu wa maonyesho hayo ambae Ni mkurugenzi wa kampuni ya kilifea production company LTD Dominic shoo amesema kuwa maonyesho hayo yatakuwa yanafanyika kila mwaka na lengo lake Ni kwa ajili ya kuwashirikisha Wakulima na kutangaza mazao yao.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Taha Jackline Mkindi amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuendeleza sekta hiyo hapa nchini.
Wakizungumza kwa niaba ya washiriki wa maonyesho hayo mhandisi Hamisi Kipalo kutoka bandari ya Tanga amesema kuwa wanaendelea na Mradi wa uboreshaji wa bandari kwa awamu ya pili kwa ujenzi wa gati namba 1 na 2 lenye urefu wa mita 450 ambao unatekelezwa na mkandarasi kutoka China akisimamiwa na mhandisi mshauri kampuni ya Niras kutoka Denmark akishirikiana na kampuni ya kitanzania ya Anova.