Walimu shinyanga watakuwa kutimiza wajibu wao kwa kujibu wa sheria

 Katibu wa Chama cha Walimu Shinyanga,  Mwalimu Allen Kizito akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga
Walimu wanachama wa CWT wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga ( hayupo pichani)

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Chama cha walimu Tanzania CWT katika Manispaa ya Shinyanga kimewakumbusha walimu kuhusu msingi wa kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za kazi.

Wameyasema hayo leo kupitia risala yao iliyosomwa na katibu wa CWT Wilaya ya Shinyanga Mwalimu Allen Kizito Shuli kwenye  mkutano mkuu wa nusu mhura kwa kipindi cha miaka mitano katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa sule ya msingi Buhangija.

Wamesema chama cha walimu Tanzania kitaendelea kuwakumbusha walimu kuhusu wajibu wao wa kutimiza majukumu kwa juhudi na maarifa

“Kupitia mkutano mkuu huu CWT bado kinazidi kuwatia shime walimu wote  kuwakumbusha waendelee kutimiza wajibu wao kwa juhudi na maarifa wakizingatia sheria, taratibu na kanuni za kazi”.

Katibu Mwalimu Shuli ameeleza pia lengo la la mkutano huo mkuu wa CWT Wilaya ya Shinyanga, kwamba umejikita kupokea taarifa ya utendaji wa kazi za chama kwa kipindi cha Miaka miwili na nusu tangu uchaguzi mkuu ulipofanyika 2020 ikiwa ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya fedha (mapato na matumizi) kwa kupindi cha kuanzia Mei 2020 hadi Septemba 2022.

Aidha pia ameeleza kuwa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Shinyanga ni utekelezaji wa tamko la umoja wa mataifa juu ya haki mbalimbali za binadamu Duniani ikiwemo na Nchi ya Tanzania.

Wametumia nafasi hiyo kumuomba mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kushughulikia changamoto zinakwamisha walimu huku wakisisitiza nidhamu, uwajibikaji na utii kwa walimu.

“Chama cha walimu Tanzania tunasisitiza sana nidhamu, uwajibikaji na utii kwa walimu wote wakiwemo wanachama wetu, tunakemea vitendo viovu hasa vile vya kudhalilisha wanafunzi wetu, wizi na matukio ya mitihani, ulevi na mikopo ya kupindukia lakini pia CWT tunaahidi kuendelea kushirikiana na wewe mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kuendelea kuwaelimisha walimu ili kuondokana na matokeo ya vitendo hivi”.amesema katibu Shuli

“Yapo mambo kadhaa ambayo tunakuomba mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga usaidie kuyaondoa kwa walimu wetu namba moja wapo walimu waliopunjwa madaraja yao toka Mwaka 2013 hadi 2022 jambo hili limesababisha walimu walioanza kazi pamoja kutofautiana mishahara na hata walimu waliotangulia kazini kuzidiwa mishahara na wanafunzi wao bila kuhusisha vigezo cha elimu zao”.

“Walimu wanaokaribia kustaafu na hawakupewa madaraja inavyostahili kupewa daraja moja kwa mujibu wa barua ya katibu mkuu utumishi kumbukumbu namba FA 97.228.01.12 ya tarehe 30 Mei,2022 wapo walimu sita ndani ya Manispaa yetu waliguswa na waraka huu na wawili kati yao walifanikiwa kupata madaraja yao na kurekebishiwa mishahara yao.”

“Mapunjo ya nauli na posho ya kujikimu kwa walimu wapya walioajiriwa kwenye Manispaa yetu ambapo walilipwa kwa utaratibu wa zamani badala ya maelekezo mapya ya serikali”.

“Mapunjo ya Mishahara kwa walimu wanayodai serikali tangu Mwaka 2013 hadi 2022 lakini pia fedha za uhamisho, nauli na matibabu zinazodaiwa kwenye Halmashauri yetu”.amesema katibu wa CWT Wilaya ya Shinyanga Allen Shuli

Katika risala hiyo pia wameishukuru tume ya utumishi wa walimu idara ya elimu msingi na sekondari pamoja na uthibiti ubora kwa kujivika majukumu ya ulezi katika kuhakikisha usalama wa walimu kazini.

Wameziomba idara zote zinazomuhudumia mwalimu kujiwekea kipaumbele na kuhakikisha shida za walimu zinatatuliwa kwa wakati huku wakiishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mpango wa kuondoa kero za watumishi.

Akizungumza mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura pamoja na mambo mengine amesisitiza suala ya uwajibikaji kwa walimu huku akiahidi kuendelea kutatua changamoto zote zinazowakabili walimu.

“Rai yangu kwenu ninyi kamati tendaji na wajumbe wa mkutano huu mkuu ambao ni viongozi huku mlikotoka niwaombe twende tukasisitize suala la uwajibikaji kupitia uwajibikaji ndiyo jambo pekee linaloenda kutujengea heshima ya haraka lakini pia heshima ya kuduma, kwenye haya madai itafika mahara yatakwisha mimi niendelee kuwaomba chama cha walimu muendelee kuja kuna yale ambayo tumeshayatatua na mengine bado tutayashughulikia moja baada ya lingine  na tunatambua thamani yenu na ambacho naweza kuahidi kupiti kikao hiki tutaendelea kuwaheshimu, kuthamini na tutafanyakazi kwa pamoja”. Amesema Dkt Satura

Aidha kupitia mkutano huo Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga Mathias Balele ametumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuwapa walimu marupurupu ya kufundishia yaani posho (Teaching allowance) huku akimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura kwa usimamizi wake mzuri.

“Nakupongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kaka yangu Jomaary Satura kwa kweli  wewe ni mtu wa pekee sana siyo vizuri kujisifia lakini ni vibaya kujipuuza sisi Shinyanga sasa tuko vizuri mimi siyo nabaa wala mtabili lakini Mungu atakufikisha mbali vitendo vyako vinasema, vitendo vyako vinaongea mji huu mbali na kuwajari watumishi hata mji wa Shinyanga unasema tumepata mtumishi mimi nikushukuru sana madaraja yanapanda lakini sasa tuongeze kasi ya mapunje kwahiyo tunaendelea kuomba tukipata kateaching allowance katatusaidia sana kwa sababu hakuna sehemu nyingine ya kipato sisi walimu tofauti na mshahara lakini pia tunaiomba serikali itupe elimu zaidi kuhusu kikokotoo”.amesema Mwenyekiti Balele

Naye Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Shinyanga Meshack Mashigala pamoja na kumpongeza mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomary Satura amesema sipo kesi mbalimbali wamekuwa wakizipata zinazowakabili walimu hivyo ameiomba serikali kuzishughulikia mapema ikiwemo walimu kupewa nauli kabla ya kwenda likizo tofauti na inavyofanyika kuwa mwalimu anapewa hela ya nauli baada ya kutoka likizo.

Chama cha walimu Tanzania (CWT) ni chama pekee cha wafanyakazi chenye nguvu na mafanikio makubwa katika kuwaunganisha, kuwatetea, kuwalinda, na kuwahudumia wanachama wake na walimu wote kwa ujumla.

Chama cha walimu kupitia wanachama wake kinaendelea kuimarisha kiuchumi na kubuni mbinu za kuboresha uchumi wa walimu kupitia taasisi za kifedha (Benki) hasa baada ya kuanzisha Benki ya walimu ambayo imekuwa chachu ya kupunguza masharti ya mikopo na riba tangu ilipoanzishwa Mwaka 2016.