Na. Elinipa Lupembe.
Walimu wa shule za sekondari halmashauri ya Arusha wametakiwa kuacha kufundisha kwa mazoe badala yake, kuongeza kasi, juhudi na maarifa katika ufundishaji kwa kutumia kutumia mbinu za kisasa, ili kuendsna na wakati lengo likiwa kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi pamoja na kupandisha hali ya ufaulu kwa wanafunzi kwa shule za halamshauri hiyo.
Rai hiyo imetolewa na kamati ya Mitihani ya halmshauri hiyo, wakati wa kikao kazi cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne ya mwaka 2020, kilichowakutanisha wakuu wa shule, walimu wa taaluma wa shule zote za sekondari pamaja na waratibu wa Elimu wa kata zote za halmashauri ya Arusha, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi ya Green Acress.
Kamati hiyo ya mitihani imetoa rai hiyo mara baada ya baadhi ya wakuu wa shule na walimu wa taaluma waliofanya vizuri kudilishana uzoefu, kwa kuelezea mbinu wanazotumia kufundisha, zinazosababisha matokeo mazuri katika shule zao.
Mwenyekiti wa kamati ya mthihani halmashauri ya Arusha na mkurugenzi mtendaji, Saad Mtambule, amewataka wakuu wa shule na waratibu elimu kata, kufuatilia utekelezaji wa shughuli za ufundishaji na nidhamu kwa walimu na wanafunzi, kwa kuhakikisha kila mmoja anatekeleza wajibu na majukumu yake ya kila siku,mjambo ambalo litapandisha taaluma na kuongeza ufaulu.
“Mbinu hizi zilizotolewa na walimu walifanya vizuri, si mbinu mpya basi ni kiasi cha walimu kuacha kufundisha kwa mazoea na kuzifanya mbinu hizo kwenda na wakati wa sasa, kiuhalisia changamoto za shule zetu zinaoendana, niwatake walimu walimu kutumia changamoto hizi kuwa fursa na kuamua kujiwekea malengo kwa kujitoa, kufundisha, kupima na kutahmini matokeo ya utendaji, kufuatia malengo mliyojiwekea” amesisitiza Mkurugenzi huyo
Aidha walimu hao wa shule zilizopata matokeo mazuri, wameweka wazi kuwa, shule zao zinazimejikita katika kufanyakazi kama timu, kwa kuwaandaa wanafunzi kitaaluma na kinidhamu, huku walimu wakihakikisha wanafundisha mada zote na kukamilisha kwa wakati na kutoa mazoezi, majaribio na mitihani ya mara kwa mara kwa kuwafuatilia pamoja na kufanya tathmini ya matokeo ya upimaji huo.
Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru mwalimu Denis Otieno,amefafanua kuwa licha ya kuwa shule ya sekondari Ilboru inapokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu, bado shule inafanya juhudi za ziada za ufundishaji ili kuhakikisha wanafunzi hao, wanafanya vizuri katika masomo yao, tangu wanapoingia shuleni hapo mpaka kufanya mitihani yao ya mwisho.
“Tumepanga safu ya ufundishaji kimasomo kupitia kila idara, safu ambayo inahakikisha masomo ya idara husika yanafundishwa ipasavyoa ‘effectively’, huku wanafunzi wakipewa mazoezi, majaribio na mitihani ya kutosha, pamoja na kuwa na idara ya ukaguzi na upimaji inayofuatiliaji na kukagua utekelezaji wa kazi zote za kitaaluma na nidhamu kwa walimu na wanafunzi” amefafanua mkuu huyo wa shule
Hata hivyo wakuu wa shule ambao shule zao hazikufanya vizuri, wameeleza kuridhishwa na kikao kazi hicho, kilichowapa mwanga na uzoefu kutoka kwa shule nyingine, uzoefu ambao wameahidi kuufanyia kazi, lengo likiwa ni kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu katika shule zao.
Awali katika kiako kazi hicho, uongozi wa halmashauri ya Arusha, umewapongeza, wajumbe wa kamati ya mitihani, Idara ya elimu sekondari, Waratibu Elimu kata, Wakuu wa shule, walimu wa taaluma pamoja na walimu wote kwa ujumla, kwa kuwezesha halmashauri hiyo kuendelea kupata matokeao mazuri kwa mitihani ya taifa ya kidato cha pili, cha nne na cha sita mwaka hadi mwaka, , na kuwataka kujipanga kutokomeza alama sifuri.
Kikao kazi hicho cha tahmini, kiliambatana na utoaji wa zawadi za pongezi kwa Wakuu wa shule 3 zilizofanya vizuri katika halmashauri hiyo, pamoja na walimu waliofaulisha masomo yao kwa alama A, B na C, kwa kupewa vyeti na pesa taslimu huku shule zilizofanya vibaya zikipewa vyeti vyenye rangi nyekundu kuashiria hatari (tafsiri isiyo rasmi).
Kwa mwaka wa masomo 2020, jumla ya wanafunzi 4,881 walifanya mtihani wa kidato cha nne kutoka shule 49 za halmashauri hiyo,na ufaulu wa jumla ukiwa ni asilimia 92.65 kufuatia malengo ya halamshauri ya kufikia asilimia 90, huku ubora wa ufaulu ukifikia asilimia 41.73 kwa wanafunzi waliopata daraja la I mpaka la III.
Wakuu wa shule, walimu wa taaluma shule za sekondari halmashauri ya Arusha, wakifuatia mijadala mbalimbali wakati wa kikao kazi cha tathmini ya matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 kwa shule zote za halmashauri ya Arusha |
Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru, mwalimu Denis Otieno, akielezea mbinu bora wanazotumia kupata matokeo mazuri kwa watahiwa wa kidato cha nne katika shule yake. |