*wananchi wa mwasonga wamtaka ndugulile kufuatilia kilio cha barabara ya lami ya kibada-mwasonga

Na Mwandishi Wetu

Wakazi wa Mwasonga leo tarehe 2 Oktoba  2021 wamefanya kikao na Mbunge wa Kigamboni Mhe. Faustine Ndugulile (Mb)  kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za eneo hilo ikiwa ni pamoja na umeme, maji safi, ulinzi na barabara za mitaa na Barabara kuu ya Kibada-Mwasonga.

Kupitia kwa Mwenyekiti wa kikao hicho Bw Osphart Chenza, wakazi wa Mwasonga walilalamikia ubovu wa barabara ya Kibada-

Mwasonga na kutotekelezwa kwa ahadi ya Rais wa awamu ya 5 Hayati Dkt John Pombe Magufuli ya kutumia Tsh 90 Billioni kwa ajili ya barabara za Wilaya ya Kigamboni. 

Akijibu hoja hizo, Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) alisema kuwa anatambua barabara hiyo ni muhimu sana kutokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda unaoendelea kwenye Kata ya Kisarawe II. Alisema kuwa Tsh 90 Billioni iliyotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2019/2020  hazikutolewa na Serikali. 

Hata hivyo, Mhe. Ndugulile alisema  kuwa  Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kilomita moja kwa kiwango cha lami ifikapo mwishoni mwa mwzi Oktoba, 2021. Pia kuna uwezekano wa kuongeza kilomita nyingine mbili katika mwaka wa fedha 2021/22. 

Pia, Dkt Ndugulile alisema kuwa Wilaya ya Kigamboni ina mtandao chini ya 1% wa barabara za lami. Hivyo, anatarajia mradi wa DMDP kuongeza wigo huo.

Naye Diwani wa Kata ya Kisarawe II Mhe Issa Zahoro akijibu kuhusu changamoto za barabara za mita, alisema kuwa yeye na Wenyeviti wa Mitaa watapitia barabara zote za mitaa na kuwasilisha maombi Tarura ili ziingizwe kwenye mfumo. Aliongeza kwa kusema kuwa Kamati ya Maendeleo  ya Kata kwa kushirikiana na wadau wataendelea kuziboresha barabara zilizopo na kufungua barabara mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *