Wanawake tarime walaani vitendo vya unyanyasaji kijinsia

 Veronica  Marengo ambaye ni Afisa Kilimo Msaidizi Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tarime akiongea katika maadhimisho ya siku ya wanawake ambapo kiwilaya wilaya ya Tarime yalifanyika kata ya Mbogi Pichazote na  na Frankius Cleophac
Mbuke Makanyaga amabaye  ni Afisa biashara Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara akiongea katika maadhimisho ya siku ya wanawake ambapo kiwilaya wilaya ya Tarime yalifanyika kata ya Mbogi
………………………..

Na Frankius Cleophace Tarime.

Katika maadhimisho ya siku ya Wanawake ambayo ufanyika Machi Nane kila Mwaka  wanawake wote ulimwenguni upaza sauti huku wakilaani vikali suala la Unyanyasaji nakueleza umma nia na malengo yao kwa ajili ya Usawa katika Nyaja za Uongoz na fursa za Kiuchumi.

Mbuke Makanyaga  ni Afisa biashara Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara katika maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo kiwilaya  wilaya ya Tarime ilifanyika kata ya Mbogi ambapo alisema kuwa muda utakapofika ataenda kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Mwibara kupitia Chama cha Mapinduzi.

“Mimi kama mwanamama nitajitokeza kwa ajili ya kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Mwibara siku kipenga kikipulizwa naomba wanawake wenzangu mniunge mkono ili wanawake tuweze kujikwamua nitafanya kazi kama wengine wanavyofanya ili kuletea Wananchi Maendeleo ” alisema Mbuke.

Mbuke aliongeza kuwa Wanawake wakiamua wanaweza bila kuwezeshwa kama kauli ambazo zimekuwa zikitajwa kuwa Mwanamke akiwezeshwa anaweza bali hiyo kauli sasa hivi hisitumike kwa sababu tayari wamedhubutu kama wanawake huku akisihi wanawake kuungana pamoja ili kuchagua wanawake wenzao.

Vile vile   alihimiza  Wanawake  kuanzisha Viwanda mbalimbali huku wakiunda vikundi   kwa ajili ya  kupata mikopo huku wakifanya biashara mbalimbali ili kujiinua kiuchumi.

Kwa upande wake  Veronica  Marengo ambaye ni Afisa Kilimo Msaidizi Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tarime naye pia katika maadhimisho hayo aliwasihi wanawawake kuwaunga Mkono Wanawake wenzao watakapojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi.

“Namimi Mwanamama mwenzenu sijarudi nyuma sana pia muda ukifika lazima na mimi niwanie kiti cha Ubunge kupitia viti maalum Mkoa wa Mara  lazima sisi wanawake tuungane” alisema Veronica.

 Veronica aliongeza kuwa  kila mtu ananafasi ya kuwania uongozi bila kujali dini, kabaira ilimradi ni kiongozi mzuri anayekubalika katika jamii.

“Wanawake ni jeshi kubwa tunatunza familia tunafanya biashara hivyo tukiamua lazima tufanikiwe pia wanawake wengine tujitokeze kuwania nafasi mbalimbali” alisema Veronica.