Zafarani Madayi, Meneja mazingira Wakala wa barabara nchini TANRODS, akijibu maswali ya Mabalozi wa usalama barabarani(RSA) kutoka mikoa mbalimbali nchini walipotembelea banda la wizara ya ujenzi |
Na Seif Mangwangi, Arusha
WAKAZI wanaoishi pembezoni mwa
barabara wametakiwa kufuata sheria za usalama barabarani kwa kutojenga nyumba
karibu na barabara ili kuepuka ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea
katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa jana na
Zafarani Madayi Meneja kitengo cha mazingira
usalama barabarani wa wakala wa barabara nchini (TANROADS), ambae amesema
wamekuwa wakilazimika kujenga matuta barabarani ili kupunguza ajali za mara kwa
mara.
Amesema kiuhalisia, barabara kuu
(high way), kwa kawaida hazipaswi kujengwa matuta barabarani lakini kutokana na
uelewa mdogo wa matumizi ya barabara TANROADS wamekuwa wakilazimika kujenga
matuta ili kupunguza ajali.
Akijibu maswali mbalimbali ya
mabalozi wa usalama barabarani waliotembelea banda la wizara ya ujenzi katika
maonyesha ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika viwanja vya shekh Amri
Abeid Arusha, Zafarani Madayi amesema TANROADS imekuwa ikihakikisha mazingira ya
barabara yanakuwa salama wakati wote.
Amesema katika maonyesho hayo
wamekuja kuonyesha kazi mbalimbali zinazofanywa na TANROADS ikiwemo ujenzi wa
barabara unaoendelea ikiwemo barabara ya mzunguko wa Dodoma, Rusaunga Dodoma,
Daraja la Tanzanite(Salander Bridge), daraja la Kigogo-busisi pamoja na ujenzi
wa viwanja vya ndege.
“ Tumeweza kuandaa kazi
mbalimbali ambazo TANROADS inazifanya, wananchi wakija hapa wataelewa kazi zetu
na kujifunza umuhimu wa kutunza barabara,”amesema.
Akijibu swali kutoka kwa mabalozi
wa usalama barabarani, kuhusu madai ya kwanini madereva wasiruhusiwe kupima
mizani moja pekee badala ya kupima kila kituo, mtaalam wa mizani kutoka wizara
ya ujenzi na uchukuzi, Mhandisi Leonard Saukwa amesema kumekuwa na sababu
mbalimbali za kupima uzito wa magari ikiwemo kupata takwimu za wingi wa magari
ili kuboresha huduma za barabara.
Mhandisi Leonard Sauko akijibu maswali ya Mabalozi ya usalama barabarani kuhusu matumizi ya mizani za kupimia magari ya mizigo na abiria barabarani |
wamekuwa sio waaminifu ambapo baada ya kupima mizani moja huongeza mzigo lakini
pia wakati mwingine mzigo hucheza na hivyo uzito kuongezeka tofauti na vipimo
vya awali.
“Katika vipimo vya mizani, tumeweka
asilimia 5 ya ziada ili kusaidia kama mzigo utacheza basi itafidia kwenye hiyo
asilimia5, lakini utakuta mfanyabiashara yeye anajaza hadi zile asilimia5 za
ziada ambazo sisi tumemuwekea, akija akikutwa mzigo umezidi anapigwa faini
anaanza kulalamika, niwaambie tu kwamba sisi sio wakorofi wafuate sheria tu,”anasema.
Anasema faini ambayo imekuwa
ikitozwa kwa magari yanayoongeza uzito ni kwaajili ya kusaidia kurudisha eneo
ambalo limeathirika na sio mapato ambayo Serikali imekuwa ikiyapata hivyo watu
wanatakiwa kufanya matumizi sahihi ya barabara ili kuepuka faini hizo.