Watoto wachungwe ibada za usiku: polisi

 Joyce Joliga, Songea. 

Wazazi Manispaa ya Songea wameshauriwa kutowaacha watoto peke yao pindi wanapoenda kwenye Ibada za Usiku kwani wahalifu hutumia mwanya huo kuwaumiza watoto.

ushauri huo umetolewa na  Mkuu wa Dawati la Jinsia wilaya ya Songea Inspekta  Oscar Kitaly wakati akitoa elimu ya usalama na ulinzi wa Watoto hasa kuelekea sikukuu za Pasaka.

Alisema, Wazazi wawe Makini iwapo wataenda Ibada za usiku wahakikishe wanawaacha majumbani  watoto wakiwa na watu wazima ilikuweza kuzuia uharifu.

Alisema, Manispaa ya songea imekuwa na vitendo vingi vya ukatili wa kingono kwa watoto hasa siku za hivi karibunihivgo ni jukumu la kila mzazi na mwananchi  kumlinda mtoto .

Kwa upande wake Assistant Inspector wa polisi Abdallah Mzumbi alisema,Jeshi la polisi limeanza doria za kuwakamata Madereva ambao wanaendesha magari, pikipiki na Bajaj wakiwa wamelewa , 

kwa upande wake , DTO Songea ASP Muya Maunganya alisema wameweka mikakati kuhakikisha watoto wanasherekea salama na kurejea majumbani kwao salama.

Alifafanua zaidi kuwa, watahakikisha kila kwenye Mkusanyiko wa watoto wanaweka Askari kwa ajili ya kuwavusha watoto , pia amewataka wazazi wasaidie kuwavusha watoto Sehemu ambazo hakuna Askari.

“Tumejipanga Vizuri kuhakikisha watoto wanavuka salama barabara  na kusherekea kwa amani , pia tutahakikusha sehemu zenye watoto Bodaboda na magari zinatembea kwa mwendo unaoruhusiwa kisheria, alisema ASP Muya.