Watu 10,000 wapatiwa mafunzo ya kupinga ukeketaji wilayani ikungi mkoani singida

Wananchi
wa Kata ya Iseke, wanafunzi kutoka Shule za Ihanja, Unyangwe na
Nkhoiree pamoja na maofisa wanaosimamia mradi wa kupambana na mila
potofu za ukeketaji na ukatili wa Kijinsia wakionesha mshikamano wa
kutokomeza kabisa vitendo hivyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Kata ya Iseke wilayani Ikungi mkoani Singida juzi.
Mratibu
wa mradi wa kupambana na mila potofu za ukeketaji, Evaline Lyimo
akizungumza na wanafunzi wakati wa kuimarisha klabu za watoto mashuleni
za kupinga ukatili wa kijinsia 
na ukeketaji.
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Muhintiri, Anatory Mzuma akizungumza na wanafunzi hao.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Unyangwe wakitoa burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wanyaturu.
Picha ya pamoja baada ya kuimarisha klabu za wanafunzi.
Mratibu wa mradi huo Evaline Lyimo akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Iseke.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa mama na mtoto wa Kata ya Iseke wakitambulishwa kwenye mkutano huo.
Mwezeshaji wa mradi huo, Japhet Kalegeya akihutubia kwenye mkutano wa hadhara.
Wakina mama wakiwa kwenye mkutano huo.
Mzee Emmanuel Lie (89) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mzee Edward Migamba (68) akizungumza.
Mama Eliwanje Ibrahim akizungumza.
Mama Maria Jason akichangia jambo katika mkutano huo.
Mwanafunzi Prisca Elifaraja akielezea changamoto zinazochangia wanafunzi kupata mimba.
Wananchi wakiangalia sinema ya mafundisho namna ya kujikinga na vishawishi kwa wanafunzi kupata mimba.
 
Na Dotto Mwaibale,Singida
 
WANANCHI
wapatao 10,258 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida
wamepatiwa elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia  na ukeketaji kwa
wanawake na watoto.
 
Hayo
yalielezwa juzi na Mratibu wa mradi wa kupambana na mila potofu za
ukeketaji wilayani humo , Evaline Lyimo katika mkutano wa hadhara wa
uhamasishaji wa utetezi dhidi ya mila potofu kama ukeketaji wanawake na
wasichana na udhalilishaji wa kijinsia uliofanyika Kata ya Iseke.
 
“Tumefanikiwa
kutoa elimu ya kutokomeza ukatili huo katika Kata tatu za Ihanja,
Ikungi na Iseke ambapo jumla ya watu 10,258 wanaume wakiwa 1200,
wanawake 2400 na wale wasio wa moja kwa moja wakiwa ni 6,658 tuliwafikia
kwa kufadhiliwa shilingi milioni 40 na Shirika la Foundation for Civil
Society (FCS) ” alisema Lyimo.
 
Akizungumza
katika mkutano huo ulioenda sanjari na kampeni  ya kuimarisha klabu za
watoto wa shule za msingi na sekondari za kupinga ukatili huo ,
Mwezeshaji wa mradi huo
Japhet
Kalegeya alisema mikutano na kampeni hizo zinasaidia kutoa elimu ya
kutokomeza kabisa vitendo hivyo ambavyo vipo kinyume na haki za
binadamu.
 
Mzee
Emanuel Lie (89) alisema baadhi ya mambo yanayochangia udhalilishaji na
mimba kwa wanafunzi ni wazazi na walezi kushindwa kusimamia malezi ya
watoto wao.
 
Mkazi
mwingine wa kata hiyo, Edward Migamba (68) alisema umbali mrefu kutoka
kijijini na zilipo shule unachangia watoto kupata mimba ambapo mama
Eliwanje Ibrahim aliongeza kuwa utandawazi nao ni sababu nyingine ya
janga hilo.
 
Mwanafunzi
wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Unyangwe, Prisca Elifaraja
akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema kutembea umbali mrefu porini
wakati wa kwenda shuleni, kukosa chakula na wazazi wanapotoa adhabu ya
kuwafukuza watoto nyumbani pale wanapokuwa wamefanya makosa huchangia
watoto kujikuta wakiangukia katika vishawishi na kupata mimba na
kubakwa.
 
Mkutano
na kampeni za kuimarisha klabu hizo za watoto mashuleni  uliandaliwa na
Shirika lisilo la Kiserikali la Save the Mother and the Children of
Central Tanzania (SMCCT) na kuhudhuria na wanafunzi kutoka Shule za
Ihanja, Unyangwe na Nkhoiree ulihitishwa na sinema ya kutoa mafunzo ya
kuepuka vitendo vinavyoweza kuwashawishi wanafunzi kupata mimba.