Watu 9 wakiwemo askari wa jeshi la polisi washikiliwa kwa rushwa

 

Sehemu ya silaha walizokutwa nazo Majambazi  pichani kamanda Hamduni akionyesha Bastola mbili walizokutwa nazo Majambazi hao waliouawa katika mapambano na Askari wa Jeshi la Polisi picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Kamanda Hamduni akionyesha Bastola kwa waandishi wa habari pembeni ni Staff One Merry Kipesha akifuatilia wakati kamanda akiongea na wanahabari mapema leo jijini Arusha.

Kamanda Hamduni akiwa anaonyesha Silaha hizo kwa waandishi wa habari hawapo pichani katika makao makuu ya Jeshi hilo mkoani Arusha

Silaha walizokutwa nazo Majambazi waliouawa 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha Salim Hamdun akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Arusha akitoa taarifa ya kuuawa kwa majambazi na kushikiliwa kwa Askari kwa Rushwa katika makao makuu ya Jeshi hilo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha 

Na Ahmed Mahmoud Arusha 

JESHI la polisi mkoa wa Arusha,linawashikilia watu tisa wakiwemo askari watatu wa jeshi la polisi makao makuu Dodoma na mkoa wa kipolisi Kinondoni, kwa kujihusisha kushawishi na kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa madini  jijini Arusha

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Salum Hamduni, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni D/C mwenye namb G 5134 Heavenlight Mushi, Idara ya Intelijensia mkoa wa Kinondoni, H 1021  PC  Bryton Murumbe askari kazi za kawaida mkoa wa Dodoma,H 125 Gaspal Paulo, Idara ya Intelijensia makao makuu Dodoma.

Wengine ambao ni raia amewataja kuwa ni   Shaban Bensoni miaka 40 mfanabiashara  na mkazi wa Makole Dodoma, Joseph Damiani Chacha  miaka 43  mfanabiashara mkazi wa Ilboru jijini Arusha, Omary Alphonce  Mario miaka 43  mfanyabiashara  mkazi wa Olerien jijini Arusha, Lucas Michael Mdeme, miaka 46 mfanyabiashara,mkazi wa Engutoto, jijini Arusha na Nelson Lyimo,miaka 58 mfanyabiashara mkazi wa Kimandolu,jijini Arusha na Leonia Joseph miaka 40 Sekretari wa kampuni hiyo a madini ambae ni mkazi wa Ilboru,

Amesema uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea  na jalada limepelekwa kwa ofisi a mwendesha mashitaka na kwa upande wa askari hao wanaoyuhumiwa taratibu za kijeshi zinaendelea.

Aidha amesema kuwa watuhumiwa hao ambao ni askari walimfuata mfanyabiashara wa madini kampuni a Germs and Rock s Ventures iliyopo mtaa wa Pangani jijini Arusha, na kupokea kiasi cha shilingi milioni 10 na walikuwa wamefuata kiasi cha shilingi milioni 20 zilizokuwa zimebakia.

 Amesema kuwa askari hao walienda kumtishia mfanyabiashara huyo na kudai kuwa alikuwa hana vibali va kufana biashara a madini, ndipo polisi walipotaarifiwa  na kuwakamata watuhumiwa hao ambao walishirikiana na raia .