<
Na Mwandishi Wetu, NJOMBE
Wakazi wa kijiji cha Kitewele kilichopo mwambao mwa ziwa Nyasa chenye jamii za wafugaji,Wavuvi na Wakulima wilayani Ludewa Mkoani Njombe wanalazimika kusafirisha wagonjwa kwa machera za fimbo za miti na mhanzi umbali wa zaidi ya km 32 ili kunusuru maisha ya ndugu zao,Hatua inayosababishwa na uwepo wa barabara ambayo haipitiki kwa gari ama chombo cha moto.
Barabara hiyo inayounganisha vijiji vya Madunda,Kitewele na Nakonde ilichimbwa miaka michache iliyopita kwa mkono na wakazi wa kijiji cha Kitewele chenye wakazi zaidi ya elfu moja huku lengo kuu likiwa ni kufungua mawasiliano ambayo yaliwafanya kuishi kama watu waliojitenga.
Wakipaza sauti katika mkutano wa mbunge wa Ludewa wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi akiwemo Beno Lwiva na Kasilida Haule wanasema katika kijiji chao kuna zahanati lakini haifikiki vyombo vya moto hivyo endapo mgonjwa analetwa ama kupata rufaa hulazimika kutengeneza machera za miti na kisha kutembea umbali mrefu hali ambayo inasababisha baadhi yao kupoteza maisha wakiwa njiani hivyo wanaomba serikali ione umuhimu wa kuunga mkono jitihada walizofanya kwa kurekebisha barabara hiyo.
Ukitolewa Ufafanuzi juu ya hatua zinazokwenda kuchukuliwa ili kumaliza adha hiyo na kunusuru maisha ya wagonjwa,kilimo na sekta ya biashara katika ukanda huo Meneja wa TARURA wilaya ya Ludewa Enhad Willa amesema tayari ameitazama barabara hiyo na kuelewa maeneo yote korofi hivyo ili iweze kukarabatiwa inapaswa kusajiliwa kwenye barabara za tarura ndipo mwaka ujao itengewe bajeti ya kutosha