Mwonekano wa ziwa Duluti ( Na picha ya mtandao) |
Uongozi wa hifadhi ya ziwa duluti ambao ipo chini ya wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)umesema kuwa bado unaendelea na oparesheni kabambe ya kuwakamata wavuvi haramu(wadokozi) wanaovua samaki kutoka katika ziwa Hilo.
Hayo yameelezwa mapema jana na Peter Muyonga, mhifadhi misitu mwandamizi wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu hali ya hifadhi hiyo kwa Sasa .
Mhifadhi Peter alisema kuwa bado kumekuwepo na changamoto hasa nyakati za usiku wananchi wanaoishi karibu na ziwa Hilo kuvamia ziwa na kisha kufanya uvuvi ndani ya ziwa Hilo jambo ambalo ni hatari sana na hakuna mwananchi yeyote yule anayeruhusiwa kufanya uvuvi
Alisema kuwa kwa miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na tatizo Hilo sana lakini kwa Sasa tatizo Hilo limepungua ingawaje bado oparesheni za kuwabaini wote wanaoendeleza uvuvi haramu kukamatwa
“Tumeweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwabaini watu Hawa ambao wanatumia akili na njia nyingi sana za kimagendo za kuvua samaki hatutawacha salama,oparesheni kadhaa zilishafanyika na bado tunaendeleza tukumbuke tu huu ni urithi ambao upo na unatakiwa kuendelea kuwepo kwa vizazi vijavyo”aliongeza
Pia aliwataka wananchi ambao mara zote ambao wanauziwa samaki ambao wamevuliwa na wavuvi harama hao kuachana na tabia ya kununua samaki hao kama kitoweo badala yake wawe mabalozi wazuri wa kutangaza uzuri wa ziwa Hilo ambalo ni kivutio kikubwa Cha utalii.
Akiongelea hali ya ziwa Hilo kwa Sasa ambalo ni kivutio kikubwa Cha utalii kwa mkoa wa Arusha,alisema kuwa idadi ya wataliu imeongezeka kwa Kasi kubwa Huku ongezeko Hilo likijunuisha watalii wa ndani tofauti na Miaka michache iliyopita
Alitolea mfano kuwa katika miaka ya 2016,2017 watalii wa ndani ilikuwa ni 3400 Huku watalii wa nje wakiwa ni 5260 na wakati kwa Sasa idadi ya watanzania ambao wanatembelea hifadhi hiyo imeongezeka
Alisema kuwa lengo halisi ni kuhakikisha kuwa watalii wa ndani wazidi kiasi Cha elfu tano jambo ambalo linawezekana kwa kuwa hifadhi ya ziwa Hilo ni kwa ajili ya kuenzi utalii