Wazazi acheni tabia ya kuwalaza watoto wenu na wageni wanao kujua majumbani mwenu wanawatendea watoto ukatili

 

Uzinduzi wa Kampeni ya “MLINDE MTOTO WA KIUME” Pichani ni tisheti imebeba ujumbe huo pamoja na Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika 2022

Inspekta wa Polisi Tadei Tarimo ambaye pia ni Polisi Kata ya Ngarenaro,Mkurugenzi wa Taasisi ya Vuka Initiative wakiwa katika Picha ya pamoja na watendaji wa Taasisi hiyo katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika 15june2022 katika kata ya Ngarenaro Jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Vuka Initiative bi Veronica Ignatus Akiwa ameshikilia bango lenye Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika Kata ya Ngarenaro.15juni 2022

Wa kwanza kushoto ni diwani wa kata ya Ngarenaro Isaya Doita Harry  ,akifuatiwa na mgeni rasmi wa Diwani wa Kata ya Moshono Miryam Kisawike,pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vuka Initiative Vero Ignatus wakikata keki ishara ya Uzinduzi wa Kampeni ya “MLINDE MTOTO WA KIUME”

Mkurugeni wa Taasisi ya Vuka Initiative akimlisha keki mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya MLINDE MTOTO WA KIUME”iliyofanyika 15juni2022 kwa ngazi ya kata ya Ngarenaro 

Mkurugenzi wa Vuka Initiative bi Vero Ignatus akiendelea na kugawa keki kwa meza kuu Mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘MLINDE MTOTO WA KIUME”iliyofanyika siku ya Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Ngazi ya Kata ya Ngarenaro

Baadhi ya Wanafunzi walishiriki katika siku ya mtoto wa Afrika Kata ya Ngarenaro iliyoambatana na uzinduzi wa Kampeni ya MLINDE MTOTO WA KIUME”ambayo ilifanywa na Taasisi ya VUKA INITIATIVE

Baadhi ya vijana kutoka Taasisi ya Vuka Initiative wakiwa wameshiriki maandamano kwaajili ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika ngazi ya kata Ngarenaro 15 Juni 2022

Baadhi ya Wanafunzi walishiriki katika siku ya mtoto wa Afrika Kata ya Ngarenaro iliyoambatana na uzinduzi wa Kampeni ya ”MLINDE MTOTO WA KIUME”ambayo ilifanywa na Taasisi ya VUKA INITIATIVE


WAZAZI ACHENI TABIA YA KUWALAZA WATOTO WENU NA WAGENI WANAO KUJUA MAJUMBANI MWENU WANAWATENDEA WATOTO UKATILI

 Na.Mwandishi wetu Arusha

Wazazi
na walezi wameaswa kutokuwalaza  watoto wao na wageni wanapotembelea
majumbani mwao kwani baadhi yao  wanawatendea watoto hao Ukatili bila
wao kujua

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
shirika lisilo la kiserikali la  Vuka Initiative Bi.Veronica Ignatus 
walipokuwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyoambatana na uzindua Kampeni ya “MLINDE MTOTO wa KIUME” Kata ya
Ngarenaro 15/6/2022 yenye Lengo la kuwakumbusha Wazazi umuhimu wa 
kuwajengea watoto msingi imara kwani ndiyo Baba wajao

“Tusipowajengea
msingi imara watoto wetu haswa wakiume tutakuja kuwa na familia za aina
gani?tukiwaacha watoto wetu bila kuwalinda wakalawitiwa tutakuja kuwa
na Viongozi wa aina gani jamani ?alihoji “

“Hakuna
kuaminiana ni kheri uchukiwe na ndugu lakini uponye kizazi chako,hao
mnaowaona wema na kuwakaribisha na kuwalaza na watoto wenu , wakati
mwingine wamekuwa wakiwatishia watoto na wao kuingiza woga kusema
vitendo vya kikatili wanavyotendewa”

Bi
Veronica
alisema kwamba asilimia kubwa ya watoto wanatendewa Ukatili na
ndugu wa karibu waliopo majumbani mwao,mbapo kwa asilimia kubwa ni ndugu
wa mume au mke au marafiki ambao familia hizo zimewaamini na
kuwakaribisha

Amesema hali hiyo ya Ukatili  kwa
watoto inakuja katika kipindi hiki ambacho wazazi na walezi wengi
wanatajwa kutokuwa karibu na watoto wao, wengi wakijihusisha na kusaka
maisha bora ili kukidhi mahitaji ya msingi ,huku wakikosa haki ya  haki
ya kuwasikiliza.

“Mgeni Kama ameweza
kijisafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine anakuja kutembelea
nyumbani kwako, na unafahamu kuwa nyumba yako haina vyumba vya kutosha
kumkimu kwanini usimtafutie nyumba ya wageni akapumzike huko hadi siku
atakavyoona vyema atakavyoondoka?”

Akizungumza mgeni rasmi katika
Maadhimisho hayo yaliyofanyika kikata diwani wa kata ya Moshono Miryam
Kisawike aliwataka Wazazi kuwa makini katika hatua za ukuaji wa mtoto
kwani kufanya hivyo kutaepusha hatari nyingi ambazo zingempata mtoto.
 
”Watoto wetu ni tunu ambayo Mungu ametupa tuitunze,sasa mzazi unapokuwa bize umjali huyu mtoto unadahania ni nani atakusaidia kumlea? tuwe wakweli unaposikia mtoto ametendewa ukatili wa kulawitiwa au kubakwa kwakweli inaumiza sana sana,hebu jamii yote tuungane kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama ”alisema Miryam Kisawike

Kwa
uande wake Inpekta Happy Adinani Mshana kutoka Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha,
amewaonya Wazazi kuacha tabia ya kupoteza ushahidi wa kesi kwa kutetea
uovu,kwa sababu ya kulinda hadhi ya familia,Sambamba na baadhi ya
waalimu kuacha kutoa taarifa pale mmoja wao anapomfamyia mwanafunzi
ukatili kuacha tabia hiyo Mara moja.

Sambamba
na hayo aliwataka Wanafunzi kuacha tabia mbaya ya kuingiliana kinyume na
maumbile kwani baadhi yao wamekuwa wakitunika kuwaingilia watoto wadogo
wa shule za msingi jambo ambalo ni baya na linaharibu malengonyaonya
kuja.akuwa baba Bora wa baadae.

“Hatufichani
nyie Wanafunzi wa sekondari mnanielewa kwani baadhi yenu mmekuwaa na
tabia mbaya ya kutumika kwa wadogo wenu wa shule ya msingi,Leo unafanya
hicho kitendo hicho ni kibaya Leo na kesho unafanya kitendo hicho
unaharibu malengo yako ya kuja kuwa baba Bora wa baadae”Alisema.
 
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ngarenaro Isaya Doita Harry aliwashukuru wageni wote walioshiriki katika maadhimisho hayo na kusema kuwa ukatili wanaofanyiwa watoto haukubaliki kamwe,hivyo jukumu kla kuwalinda watoto ni la kila mmoja kuhakikisha watoto wanakuwa salama
 
”Wazazi tunawaomba sana kutoa ushirrikiano pale ambapo mtoto amefanyiwa ukatili wakati mwingine hao wanaowatendea watoto wenu ukatili mnawafahamu ila mnawaficha hamtaki wajulikane mnawatunzia siri na kumaliza kesi hizo kimyakimya kifamilia,niwaambie ukweli mnawaumiza watoto wenu,tupeni ushirikiano ili watoto wabakie salama na kutuimiza ndoto zao za baadae”Alisema Doita
 
Aidha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka 16juni ila kwa kata ya Ngarenaro yalifanyika 15juni 2022 yakiwa yamebeba Kauli mbiu isemayo ”Tuimarishe Ulinzi wa Mtoto,Tokomeza Ukatili Dhidi yake”Jiandae kuhesabiwa