Waziri mkuu majaliwa awafunda watumishi wa jiji la arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Waziri mkuu kasimu Majaliwa amewataka watumishi wa umma kwenda moja kwa moja kwa wananchi na kuachana na tabia ya kukaa maofisini

Ameyasema hayo mapema Leo kwenye kikao na watumishi wa umma kutoka katika jiji la Arusha,kikao kilichofanyika katika ukumbi Wa Aicc

Majaliwa amesema kuwa mtumishi wa ummma anatakiwa kuwafuata wananchi kwenye vijiji na Wala sio kukaa maofisini pekee

Aliendelea kwa kusema kuwa wanapoenda kwa wananchi wanatakiwa kwenda na Agenda maalumu ambayo itawakutanisha hivyo na kwa kufanya hivyo kutapunguza kero

Aliongeza kuwa huu sasa ni wakati wa kila mtumishi wa umma kuhakikisha anafanya kazi kwa kufuata maadili na taratibu za kazi

“Tuache mazoea,na tunatakiwa kufanya kazi kwa kufuata taaluma,tuache ubaguzi katika kutoa huduma,ni wajibu wetu sasa kuwahudumia hawa wananchi tena kwa staha kubwa sana”aliongeza

Katika hatua nyingine aliwataka viongozi wa ofisi ya mkuu wa mkoa,wilaya pamoja na jiji kuhakikisha kuwa wanakuwa na ushirikiano mzuri

Alidai kuwa mpaka sasa kumekuwa na mawasiliano mabaya baina ya viongozi hao ila kwa sasa wanatakiwa kuwa na lugha moja tu ya kuwasaidia wanachi.

“Lazima mkae Kama timu mfanye kazi pamoja na mnatakiwa mjue nani ni nani na msidharauliane mawasilino ni muimu sana”aliongeza 

“Nimemsikia Mbunge hapa akiongea jambo na ninadhani hapa hamna mawasiliano mazuri maana lingewasilishwa huko,Arusha kuna makundi mengi ambayo mengine yanahusisha hadi viongozi wa taifa “aliongeza

Katika hatua nyingine aliwataka baadhi ya watumishi wa umma kuachana na tabia ya kuchukua baadhi ya zabuni ambazo zinatangazwa na halmashauri

Majaliwa alisema viongozi wanachukua zabuni mbalimbali inasababisha kuwepo na migogoro ambayo sio ya lazima