Waziri ndumbaro asisitiza matumizi ya tehama kutoa elimu kwa umma

 Na  Magesa Magesa,Arusha

WIZARA ya Katiba na Sheria, imesisitiza matumizi ya  teknolojia  ya habari na mawasiliano (Tehama), katika kutoa  elimu kwa Umma kuhusu Katiba mpya na uwasilishaji wa mashauri mbalimbali kwenye mahakama nchini hali itakayosaidia kuwapunguzia gharama na muda mwingi wananchi wanapofuatilia huduma za kisheria.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas
Ndumbaro,alipokuwa akifungua kikao kazi cha mafunzo ya matumizi ya mifumo ya Tehama kwa Wasajili wasaidizi wa huduma za sheria, maafisa magereza, taasisi za huduma za msaada wa  sheria, wataalamu wa sheria na watumishi kutoka Tamisemi,.

Amesema kuwa katiba bajeti ya mwaka 2022/2023 Wizara hiyo  imeweka vipaumbele 14,kimojawapo cha kipaumbele hicho ni matumizi ya tehema, katika mifumo yote ya sheria ili matumizi yote yaende kidigitali .

Waziri Ndumbaro,amesema Mhimili wa mahakama umefanikiwa sana katika matumizi ya Tehama swala la Tehama limekuwa vizuri likifungamanishwa na haki ikipatikana kwa haraka na kuondoa usumbufu.

Amesema wizara inajukumula kutoaelimu hasa yaKatiba mpya ili watu waijue historia yake ili wawe nauelewa mkubwa ,ambapo itatumia Tehama kutoa elimu hiyo kutokanana asilimia kubwa ya Vijana kutumia mitandao ili waweze kuidai.

Amesema mhimili wa mahakama nchini umepanga sera kila mkoa kuwa na mahakama kuu na kila tarafa kuwa na mahakama ya mwanzo.

Amesisitizakuwa matumizi yaTehama ni ya lazima kwa kuwa hayaepukiki na kila kitu kitakuw akinapatikana kwenye mitandao ikiwemo elimuya sheria

 Amesema kuwa agenda kuu nisheria na tehama na wizara imepiga hatua kubwa sana ingawa hawajafikia wanakoenda katika matumizi ya Tehama

Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan,ameshatoa maelekezo kwa Wizara hiyo kuondoa usumbufu kwenye mashauri ya hakijamii.

Awali akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria, Kaimu Katibu tawala mkoa wa Arusha, David Lyamongi,amesema kuwa Mawakili binafsi wamekuwa ni msaada mkubwa katika maswala ya kisheria ambapo wamekuwa wakitumika kutatua kesi mbalimbali kwa wananchi na hivyo kuondoa usumbufu na haki imekuwa ikipatiukana .

Amesema kuwa kupitia mawakili hao Yatima na Wajane wamekuwa  wakipata msaada hivyo umefikawakati wapewe kipaumbele na nguvu ya kisheriailikuweza kukamilisha maswala mbalimbali kwa muda  .

Nae mkuu wa Kitengo cha Tehama wizarani, Gabriel Omary, amesema mafunzo hayo ya utumiaji wa huduma ya Tehama  yana lengo la kuwezesha wananchi kutumia huduma ya mtandao ilikuweza kupata haki kwa wakati na haraka ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia gharama pindi wafuatapo huduma za kisheria