Zifahamu sifa na ubora wa simu za tecno kwa mwaka huu wa 2020.

 Na Mwandishi Wetu.

Mwaka 2020 karibia unafikia ukingoni, bila shaka mwaka huu umekuwa ni mwaka wa

changamoto nyingi kwa duniani nzima, lakini pamoja na hayo mwaka 2020 ni mwaka ambao

umefanya teknolojia kutumiwa na watu wengi sana duniani ikiwa pamoja na ujio wa bidhaa bora

ambazo zimerahisha maisha ya wengi.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha sifa pamoja na ubora wa simu mpya za TECNO

zilizotoka kwa mwaka 2020. Kama ulikuwa unafikiria kununua simu ya yoyote ya TECNO

iliyotoka mwaka 2020 basi pengine list hii inaweza kusaidia kufanya manunuzi kulingana

mahitaji yako.

TECNO Camon 16 Premier

Kama unatafuta simu ya TECNO yenye ubora karibia kila mahali TECNO Camon 16 Premier ni

simu bora sana, simu hii inakuja na kamera bora huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 na

nyingine zikiwa na Megapixel 8 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja ambazo ni

low-light sensor. Kamera hizi zinakuja na teknolojia ya image stabilization ambayo inakusaidia

kuchukua video za 4K zilizotulia zaidi. Mbali na hayo simu hii pia inao uwezo mkubwa wa

kuchukua picha na video bora sana hata wakati wa usiku.

                                                        PICHA YA CAMON 16 PREMIER

Kwa upande wa kamera ya mbele Camon 16 Premier inakuja na kamera mbili za selfie, kamera

moja inakuja na Megapixel 48 ambayo ni wide sensor na nyingine ni Megapixel 8 ambayo hii ni

ultrawide. Kamera hizi zote kwa pamoja zina kuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p.

TECNO Camin 16s

TECNO Camon 16s ni toleo lingine la simu mpya za Camon 16 mwaka 2020, toleo hili ni tofauti

kidogo na toleo la Camon 16 Premier, kwani kwa bei nafuu zaidi utapata simu hii yenye kamera

nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48, kwa kutumia simu hii unaweza

kuchukua video hadi za 1080p@30fps. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya

Megapixel 8 huku nayo ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.

                                                          PICHA YA CAMON 16S

TECNO Camon 15 Premier

Camon 15 Premier ni toleo jingine la simu za Camon, simu hii imetoka mapema mwaka 2020 na

inakuja na sifa bora, Camon 15 Premier ni simu inakuja na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi

wa ndani wa GB 128 huku ikiwa na kamera kuu yenye uwezo wa Megapixel 64 na kamera ya

selfie ikiwa na Megapixel 32.

                                               PICHA YA CAMON 15 PREMIER

TECNO Camon 15

Camon 15 ni toleo jingine la ambalo pia linakuja na sifa nzuri ikiwa pamoja na kamera kuu ya

megapixel 48, pamoja na kamera ya nyuma ya selfie ya Megaixel 16. Kama unataka kuiliki simu

ya Camon 15 yenye kamera nzuri basi unaweza kununua simu hii ya Camon 15.

                                                          PICHA YA CAMON 15

TECNO Pouvoir 4

TECNO Pouvoir 4 ni simu nyingine bora kutoka kampuni ya TECNO iliyotoka mwaka 2020,

simu hii ni bora hasa kama wewe unataka simu yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda

mrefu, simu hii inakuja na battery kubwa ya 5000 amh, battery ambayo inaweza kudumu na

chaji siku nzima kulingana na matumizi yako.

                                                      PICHA YA POUVOIR 4

TECNO Pouvoir 4 Pro

TECNO Pouvoir 4 Pro ni toleo lingine ambalo linakuja na uwezo mkubwa wa battery lakini

zaidi ya hapo simu hii pia inakuja na sifa nzuri kama uhifadhi wa ndani wa GB 128 pamoja na

RAM ya GB 6. Kama unataka uwezo zaidi na simu yenye kudumu na chaji zaidi basi simu hii ya

TECNO Pouvoir 4 Pro ni simu bora kwako.

                                                      PICHA YA POUVOIR 4PRO

TECNO Spark 5 Pro

TECNO Spark 5 Pro ni simu nyingine kutoka TECNO iliyotoka mwaka 2020, simu hii inakuja

na kioo kikubwa cha Inch 6.6 ambacho kina resolution ya hadi 720 kwa 1600 pixels. Mbali ya

kuwa simu hii inayo kioo kikubwa pia inakuja na battery bora yenye uwezo wa kudumu na chaji.

Bila kusahau Spark 5 Pro inakuja na kamera nne, kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na

nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja na nyingine ikiwa ni QVGA.

                                                       PICHA YA SPARK 5PRO

TECNO Spark 5

TECNO Spark 5 ni toleo lingine la Spark 5 Pro, simu hii nayo ni moja kati ya simu ambayo

inapatikana kwa bei nafuu zaidi huku ikiwa na kioo kikubwa kama cha Spark 5 Pro cha inch 6.6,

pamoja na battery kubwa ya 5000 mAh. Pia simu hii inakuja na kamera nne kwa nyuma huku

kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 na moja ya mwisho

ikiwa ni QVGA. Simu hii pia ina uwezo wa resolution ya hadi 720 kwa 1600 pixels.

                                                                     PICHA YA SPARK 5

Tembelea https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/ kwa mengi zaidi kuhusiana na bidhaa za

TECNO.