Corona yapiga hodi kumbi za starehe, zaamua kupunguza idadi ya wateja

 

Na Mwandishi Wetu, Arusha.

Elimu ya afya juu ya
kujikinga na ugonjwa wa COVID-19 imeonesha kuzaa matunda baada ya
wafanyabiashara wa kumbi za starehe kuamua kupunguza idadi ya wateja wanaoingia
katika kumbi hizo.

Wakizungumza kwa
nyakati tofauti wasimamizi wa kumbi hizo wamesema lengo la kufanya hivyo linatokana
na maagizo yaliyotelwa na serikali juu ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo
kuepuka misongamano isiyokuwa na lazima.

Wamesema hatua hiyo
haijaathiri biashara kwani wanaendelea kutoa burudani kwa wateja wao kama
kawaida na kwamba kilichobadilika na idadi ya watu hivyo kuwataka wateja
kukubaliana na mabadiliko hayo.

Msimamizi wa ukumbi wa
mziki wa Orstrich uliopo Kijenge, Mathias Chuwa wamesema ukumbi wake unauwezo
wa kubeba watu mia moja kwa siku na siku za mziki walikuwa wakipata wateja kati
ya 60-80.

Anaendelea kusema kuwa
baada ya kuzuka kwa ugionjwa huo wameamua kuchukua watu wasizidi 50 lengo ni
kulinda afya za wateja wake ikiwa ni pamoja watu wanaowazunguka.

“Licha ya kuwa hatuwezi
kupata pesa au faida kama mwanzoni, lakini afya ya mwanadamu ni kitu cha muhimu
zaidi ya pesa, hivyo sisi kwa hiari yetu tumeamua kuchukua tahadhari ya
kupunguza idadi ya watu wanaingia klabuni siku za mziki” Alisema Chuwa.

Mmoja wa wasimamizi wa
klabu ya Mjengoni amesema eneo lao ni kubwa na kwamba wateja wanapata nafasi
wakati wa kucheza na hata kukaa hivyo bado hawajafikiria kupunguza idadi kwa
kuwa eneo lao ni rafiki.

“Kama unavyoona eneo
letu ni rafiki, lina ukubwa wa kutosha, lina uwazi pia, hewa ya kutosha, hivyo
kuhusu kupunguza idadi bado hatujafikiria kwa sababu bado hatujapata wateja
wengi wa kutuzidi, ikitokea tutafanya hivyo (kupunguza)” Alisema meneja huyo.