Diamond platnumz amjibu ali kiba

Diamond
Platnumz amezungumzia kilichoandikwa na msanii mwenzake, Ali Kiba
katika mtandao wake wa  kijamii wa Instagram saa chache baada ya 
kumualika kushiriki tamasha la Wasafi litakalofanyika Novemba 9, 2019.

Akizungumza jana Ijumaa Novemba Mosi, 2019 katika televisheni ya Wasafi
,Diamond alisema hakujua Ali Kiba alilenga nini, akibainisha kuwa hawezi
kuwa na chuki naye.


“Alikiba
ni kaka yangu, amenizidi umri na alianza muziki kabla yangu. Sijui
aliandika vile akimaanisha nini, yeye na mimi ni miongoni mwa
tunaoiletea sifa nchi kupitia muziki, upinzani wetu ni kwenye muziki tu,
simchukii na nina imani naye pia hanichukii.


“Mimi nimetokea maisha ya chini sana ila Mwenyezi Mungu amenibariki ndio
maana niliwashika mkono watu wengine ikiwemo Harmonize, tamanio la
WASAFI ni kuona vijana tunapeana support na kumuunga mkono kwenye vitu
ambavyo anavifanya.
“Mtu anavyofanikiwa na kuanza kushika mkono vijana wengine ni jambo
zuri, furaha yangu ni kuona vijana wengi wa Tanzania wenye talent
wanafanikiwa, pengine na mimi nisingemshika mkono, watu wasingeona
kipaji chake.
”Nimefanya kazi nyingi za Kushirikiana na wasanii, nina collabo nyingi
ndani hadi natamani nizitaje, nina ngoma inakuja na Swaelee, kuna
nyingine nimefanya na Steff London.
“Wasafi Festival itaanza mapema na kutakuwa na mashindano ya kuimba,
Mshindi atapata Tsh. Millioni 10 na nafasi ya kusainiwa WCB Wasafi,
kutakuwa na mashindano ya Dancers ambapo washindi pia watapata zawadi ya
Tsh. Million 10 na nafasi ya kufanya kazi na wasanii wa WCB.
“Juzi tu hapa nilishinda Tuzo ya Mtumbuizaji bora Siku ya Festival
nitatumbuiza kweli na hapa Nipo na Mh. Makonda Siwezi kumuangusha kwenye
mkoa wake,” amesema Diamond.