Ebitoke amvamia mlela na mpenzi wake kwa fujo mbele ya waandishi wa habari

Mchekeshaji
Ebitoke ameuvamia mkutano wa Mwigizaji Yusuph Mlela na Waandishi wa
Habari Dar es salaam na kutaka kupigana na Mlela na Mpenzi wake mpya
ambae alikua ameongozana nae kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari
ikiwa ni siku chache tu toka Mlela adaiwe kuachana na Ebitoke.


Ebitoke amesikika akisema; “Mwacheni nimwonyeshe”, huku akitukana matusi ya nguoni licha ya kudhibitwa na mabaunsa.


Kaka
wa Ebitoke naye amesikika akimwambia Mlela, “Umemuharibia maisha mdogo
wangu” huku waandishi wa habari na wasanii wenzake waliokuwepo wakibaki
wameduwaa.