Msanii maarufu wa nyimbo za injili, kizito mihigo ajinyonga kituo cha polisi

Mwanamuziki maarufu kwa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo.
Polisi ya Rwanda imetangaza kwamba msanii maarufu wa nyimbo za injili, Kizito Mihigo ”amejinyonga” Polisi wa Rwanda wanasema.
Kwa mujibu wa tangazo la polisi, maiti ya msanii huyo imepatikana katika
chumba alimokuwa anazuiliwa kwenye kituo cha polisi mtaa wa Remera,
mjini Kigali.
Polisi imesema kwamba amejinyonga siku tatu baada ya kukamatwa karibu na
mpaka baina ya Rwanda na Burundi katika kile ambacho polisi ilisema
alikuwa na nia ya kutoroka nchi na kujiunga na makundi ya waasi dhidi ya
Rwanda.
Alikuwa ameanza kufanyiwa uchunguzi kuhusu madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkataa.
Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa
kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha
raia kupinga serikali.Mwaka
2015, Bwana Kizito alikutwa na hatia kwa kosa la jaribio la kutaka
kumuua Rais Paul Kagame na kuhamasisha vurugu dhidi ya serikali na
kufungwa lakini baadae alisamehewa
Kumekuwa na hisia mseto katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha
ghafla cha msanii huyo wa muziki wa injili huku baadhi ya watu wakitaka
majibu kutoka kwa serikali.
Kizito, aliyekuwa na miaka 38 alipata umaarufu kutokana na nyiimbo zake
kama vile ‘Inuma’ unaomaanisha njiwa na ‘Igisobanuri cy’urupfu’ ambao
unaelezea kifo ni nini.
Chanzo – BBC