Act -wazalendo yatangaza uchaguzi mkuu ili kupata viongozi wapya ikiwemo nafasi ya zitto kabwe

Chama
cha ACT -Wazalendo nchini Tanzania kimefungua pazia kwa wanachama wake
wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuchukua fomu.Nafasi
zitakazogombewa ngazi ya Taifa ni kiongozi wa chama, naibu kiongozi,
mwenyekiti wa Taifa, makamu mwenyekiti Taifa – Tanzania Bara na
Zanzibar, katibu mkuu, wajumbe wa halmashuri kuu (nafasi 15) na wajumbe
wa kamati kuu (nafasi nane)

Akizungumzia
na waandishi wa habari jana Jumatatu Januari 27, 2020 katibu mkuu wa
chama hicho,  Dorothy Semu amesema uchaguzi wa viongozi wakuu utafanyika
Machi 14, 2020 ukitanguliwa na chaguzi nyingine za ngome ya wazee,
ngome ya vijana na ngome ya wanawake.