Ajali yaua watu watano kwenye daraja la mchepuko kiyegeya morogoro

Watu watano wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa, kufuatia ajali
ya barabarani baada ya Lori kubwa la mizigo, kuigonga gari ndogo ya
abiria aina ya Noah, wakati likisubiri kuvuka katika daraja la mchepuko
la kiyegeya, ambalo lilisombwa na maji mwanzoni mwa mwezi Machi.
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Machi 23, 2020, huku chanzo
kikielezwa kuwa ni kufeli kwa breki ya Lori na kupelekea vifo vya watu
wanne papo hapo na mmoja kufariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini.
Inaelezwa kuwa ajali hiyo baada ya Lori la mizigo kuligonga gari dogo
aina ya Toyota Noah wakati likisubiri kuvuka katika Daraja la mchepuo la
Kiyegeya,Morogoro na magari yote yakatumbukia kwenye shimo ambako
ujenzi unaendelea. 
Akizungumza katika eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro
Wilbroad Mutafungwa, ameeleza kuwa gari hiyo ndogo ilikuwa imebeba
abiria kutoka Dumila kuelekea Gairo na kwamba Jeshi la Polisi
linaendelea kumtafuta dereva wa Lori kwani alikimbia