Mamlaka
ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya kwa kushirikiana na
jeshi la polisi linamshikilia aliyekuwa Afisa Usalama wa Shirika la
Posta Tanzania Bw.George Arsein Mwamgambe kwa tuhuma za kusafirisha
madawa ya kulevya kwa njia ya Posta.

Taarifa
hiyo imetolewa jana Septemba 23 na Kaimu kamishina Jenerali wa Mamlaka
hiyo James Kaji, ambapo amesema kuwa mwanaume huyo walimkamata kwa
kushirikiana na jeshi la polisi na kwamba hapo awali aliwahi kutoweka
kufuatia mahojiano yaliyokuwa yakiendelea dhidi yake.

”Mamlaka
imemkamata George Mwangabe pamoja na wenzake sita wanaohusishwa na dawa
za kulevya aina ya Heroin ambapo hadi sasa uchunguzi umekamilika na
washtakiwa watafikishwa mahakamani”, amesema Kaimu Kamishina Kaji.

Kwa upande mwingine katika kipindi cha mwezi Septemba, Mamlaka hiyo
imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Heroin zaidi ya kilo moja
katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza pamoja na zaidi ya kilo 214 za
vifurushi vya dawa za kulevya aina ya mirungi, zilizokuwa zikisafirishwa
kwa njia ya Posta kutoka Arusha kwenda nchini Uingereza.