Aliyekuwa kiongozi wa brigedi ya faru apongeza ushirikiano uliopo kati ya jeshi na ofisi ya mkuu wa mkoa wa tabora

NA TIGANYA VINCENT

Aliyekuwa
Kiongozi   wa Brigedi ya Faru amepongeza ushirikiano uliopo baina ya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Jeshi la Wananchi katika utekelezaji
wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.


Kauli
hiyo imetolewa  na aliyekuwa kiongozi katika Brigedi ya Faru ,Bregedia
Jenerali Antony Chacha Sibuti wakati wa mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa
wa Tabora Msalika Makungu alipofika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
tabora kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhama Makao Makuu ya Jeshi
mjini Dodoma.


Alisema
katika kipindi alipokuwa akisimamia Brigedi ya Faru, Jeshi la Wananchi
limeweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali ikiwemo
utunzaji wa mazingira na upandaji miti katika kutekeleza agizo la Makamu
wa Rais.

Brigedia Jenerali Sibuti aliongeza kuwa ana matumaini Brigedia Jenerali
Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi yake ya kuongoza Brigedi ya
Faru ataendelea ushirikiano uliopo na kuchochea maendeleo ya eneo hilo.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alimshukuru
Brigedia Jenerali Sibuti kwa mchango wake mkubwa wa kukuza ushirikiano
kati ya Jeshi la Wananchi na Mkoa wa Tabora na kusaidia katika upandaji
miti kwa kutumia wanajeshi.
Naye Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya
kuongoza Brigedi ya Faru alisema Jeshi la Wananchi litaendelea kuunga
mkono juhudi za uongozi wa Ofisi ya Mkoa wa Tabora ya kuugeuza Mkoa huo
kuwa wa kijani kwa ajili ya kukabiliana na uharibifu wa mistu.
Alisema ataendelea kutoa Vijana wa Jeshi la Wananchi ili waweze
kushiriki katika upandaji wa miti na shughuli nyingine za maendeleo kwa
ustawi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Brigedia
Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya
kuongoza Brigedi ya Faru akifafanua jambo wakati alipomsindikiza 
aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru, Bregedia Jenerali Antony Chacha
Sibuti (katikati) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya
kuaga mara baada ya kuhamia Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine
ni Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia)  na pembeni ni
Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa.

Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (aliyesimama) akitoa maelezo
mafupi mara baada ya kukutana na aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru
,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (katikati) ambaye alifika
katika  kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuaga mara baada ya
kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine ni Brigedia
Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya kuongoza
Brigedi ya Faru na aliyepembeni ni Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa
Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa.
 

Aliyekuwa
kiongozi wa Brigedi ya Faru na kuhamia Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi
,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (wa pili kutoka kushoto) ,
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (wa tatu kutoka kushoto) ,
Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya kuongoza
Brigedi ya Faru(katikati) wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Maafisa wa Jeshi la Wananchi  mara baada ya
kumalizika mazungumzo ya aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru Bregedia
Jenerali  Sibuti kuagana na uongozi wa Mkoa wa Tabora .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *