Aliyeshiriki kutunga sheria ya kuzuia uzinzi afumaniwa akihondomola mke wa mtu

Mwanaume mmoja
nchini Indonesia ambaye alishiriki kwa kiasi kikubwa kuandaa Muswada wa
sheria ya kupinga vitendo vya uzinifu nchini humo amekamatwa akizini na
mke wa mtu.

Mukhlis bin Mudammad ni mmoja kati ya wwanachama wa baraza la
wanatheolojia ambalo lilisaidia kutunga sheria za Kiisilamu kupinga
vitendo vya zinaa pamoja na baadhi ya makosa mengi, lakini alijikuta
akicharazwa viboko 28 hadharani mbele ya kadamnasi ya watu hapo jana
siku ya Alhamisi katika Mkoa wa Aceh, Besar kufuatia kufumaniwa uzinzi
na Mke wa mtu.
Tukio hilo linamfanya, Mukhlis bin Mudammad mwenye umri wa miaka 46,
kuwa kiongozi wa kwanza wa baraza hilo kuadhibiwa na sheria hizo baada
ya kukutwa na hatia.
Mukhlis pamoja na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 33, ambao wote
wawili ni wanandoa wamepatika na hatia ya kuchepuka na kuzisaliti ndoa
zao kupitia mahaka ya Mkoawa Aceh ya ekhtilat baada ya kufumwa wakifanya
vitendo hivyo ndani ya gari katika fukwe mwezi uliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *