Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk Zainab Chaula (kulia) akizungumza na vijana waliokuwa wakiweka namba za nyumba katikaziarayakeyakukagua utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk Zainab Chaula (wa pili kulia) akishuhudia zoezi la uwekaji namba za nyumba ikiwa ni utekelezaji wa kukamilisha mpango wa anwani za makazi na postikodi Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma
Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk Zainab Chaula (kulia) akizungumza na
vijana waliokuwa wakiweka namba za nyumba ikiwa ni utekelezaji wa kukamilisha
mpango wa anwani za makazi na postikodi Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma
Na Faraja Mpina WUUM, Dodoma
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) na Taasisi
zilizo chini ya sekta hiyo zipo katika utekelezaji wa mpango mkakati
shirikishi wa kukamilisha mpango wa anwani
za makazi na postikodi unaotarajiwa kufikia halmashauri zote nchini
ifikapo mwaka 2022
ili kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kidijitali.
Akizungumza katika ziara ya kukagua uwekeaji wa namba za
nyumba katika kata Tatu za Chamwino Ikulu, Ipagala na Hazina,jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dkt.
Zainab Chaula amesema kuwa ukamilishaji wa mpango huo utarahisisha shughuli za biashara mtandao na huduma
za posta mlangoni.
“Wizara
ipo kwenye utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha kila nyumba inakuwa na
anwani ya makazi inayojumuishajina
la barabara, mtaa na namba ya nyumba, ili wananchi waweze kufikiwa
katika maeneo wanayoishi kwa urahisi na kukuza biashara mtandao na posta
mlangoni kuelekea uchumi wakidijitali”,
alizungumzaDkt. Chaula.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Wizara hiyo,
Mhandisi Clarence Ichwekeleza amesema kuwa mpango wa anwani za
makazi na postikodi unatambulika kimataifa ukamilishwaji wake
utasaidia kuongeza fursa za kibiashara na kujiajiri hasa kwa upande wa
biashara mtandao ambapo wananchi wataweza kuagiza bidhaa nakuletewa
mpaka mlangoni.
Aliongeza
kuwa utekelezajiwazoezihilounahusishaWizaraya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TAMISEMI, Halmashauri na wadau
mbalimbalia mbapo kazi inayoendelea kwasasa ni uwekaji wa namba
za nyumba katika halmashauri za jiji la Dodoma chini ya mkandarasi SUMA
JKT na Jumla ya nyumba 21,947 zitawekewa namba kati ya nyumba 30,152.
Awali akizungumza Mtendaji Mkuuwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina
Mashiba amesema kuwa ushirikishaji wa serikali na wananchi katika zoezi la
uwekaji vibao vya namba za nyumba ndio unaorahisisha kufanyika kwa zoezi hilo huku UCSAF
ikiwa imechangia shilingi milioni 60 kwa ajili ya kata tatu za Chamwino Ikulu,
Bahi na Hazina zilizopo jijini Dodoma.
Mpango wa uwekaji wa anwani za makazi na postikodi umetekelezwa katika
kata 116 nchini kati ya kata 3956, kwenye Halmashauri 18 katiya 185 nchini.
Mwitikio wa zoezi hili kwa wananchi ni mzuri kwasababu wenye manufaa kwa wananchi na Serikali katika ufikishaji wa huduma
za dharura, biashara na huduma za posta.
Alisema faida nyingine za
mpango huu kwa Serikali ni kurahisisha ukusanyaji wa kodi,
kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi na kuhudumia wananchi wakati wa dharura za
majanga ya moto na dharura ya wagonjwa.
ImetolewanaKitengo cha MawasilianoSerikalini Wizara yaUjenzi, Uchukuzi naMawasiliano (Sekta yaMawasiliano)