Apc yafanya mkutano wake wa mwaka, waandishi watakiwa kuwatenga wanaoeneza ‘udini’

Wanachama wa APC wakiwa wanajitambulisha


Na Mwandishi Wetu, APC BLOG,ARUSHA

WAANDISHI
wa habari wametakiwa kuwakataa na kuwatenga waandishi wa habari ambao
wamekuwa wakieneza masuala ya udini kupitia makundi ya Jumuiya za
waandishi kwa kuwa kuendelea kufanya nao kazi ni kutengeneza mgawanyiko
miongoni mwa waandishi na kuvunja umoja na ushirikiano ambao umekuwa
ukifanywa kwa pamoja kwa miaka mingi.

wanachama wa APC wakisikiliza hoja za mmoja wa wajumbe
Miongoni mwa wanachama wa miaka mingi wa APC Mwanaidi Mkwizu akijitambulisha mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa APC wa 2018/19
Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu akihakiki akidi ya wanachama katika mkutano mkuu wa APC wa 2018/19 uliofanyika Desemba 21, 2019 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa
Katibu Mkuu wa APC, Mustafa Leu akisikiliza hoja za wajumbe mara baada ya kumaliza kuwasilisha taarifa ya kamati ya utendaji ya APC kwa kipindi cha 2018/19
Mmoja wa wanachama wa APC Allan Isack akipitia nyaraka za Mkutano Mkuu katika Mkutano Mkuu wa APC wa wanachama 2018/19
Na Mwandishi Wetu, APC BLOG,ARUSHA

WAANDISHI wa habari wametakiwa kuwakataa na kuwatenga waandishi wa habari ambao wamekuwa wakieneza masuala ya udini kupitia makundi ya Jumuiya za waandishi kwa kuwa kuendelea kufanya nao kazi ni kutengeneza mgawanyiko miongoni mwa waandishi na kuvunja umoja na ushirikiano ambao umekuwa ukifanywa kwa pamoja kwa miaka mingi.

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano mkuu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), uliofanyika jana Desemba 21, 2019 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu amesema umoja na ushirikiano ambao APC imekuwa nao ulianza tangu miaka 27 iliyopita.

Amesema hata hivyo katika siku za hivi karibuni kumetokea baadhi ya waandishi kuanzisha masuala ya udini kupitia makundi ya wanahabari mkoani Arusha jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa hata siku moja.

Amewataka waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha kuwapuuza watu hao na kuacha kushirikiano nao kwa kuwa kufanya hivyo wataamini upuuzi ambao wamekuwa wakiueneza na matokeo yake ni kutengeneza mpasuko miongoni mwa waandishi na matokeo yake ni makubwa.

“Umoja huu wa waandishi ulijengwa miaka 27 iliyopita, lakini leo hii anatokea mpuuzi mmoja anaanza kusema kuna watu wa dini fulani wanapendelewa, naombeni waandishi muwapuuze watu wa namna hii, na tunapenda kusema kuwa wakiendelea tutawadhibiti kwa kufuata kanuni zetu za chama na katiba ya nchi ili kukomesha tabia hii,”alisema Gwandu bila kuwataja watu hao.

Katika Mkutano huo Mkuu, ambao wanachama wa APC walisomewa taarifa ya mapato na matumizi pamoja na taarifa ya kamati ya utendaji na kuzipitisha bila pingamizi lolote, pia Kamati ya utendaji iliwasilisha baadhi ya mapendekezo ya katiba ya APC na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.
  
Pia Mwenyekiti wa APC alitumia mkutano huo kutambulisha wanachama wapya ambao ni Grace Macha, Deo Moita, Mahmoud Ahmad, Vailet Lema, Zulfa Mfinanga, Amani James na Lucas Myovela na kuwataka waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha kujiunga kwa wingi na APC ili kuongeza wigo wa umoja huo.

Aliwapongeza wanachama ambao wamefanikiwa kukamilisha masomo yao kwa ngazi za stashahada na shahada na kuwataka wanachama na waandishi wote Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanajiendeleza kielimu kabla ya mwaka 2021 ambapo sheria mpya ya huduma za habari itaanza kutumika na waandishi wasiokuwa na kiwango cha elimu ya diploma watakosa sifa za kuendelea na uandishi.

Gwandu pia alitumia mkutano huo kuwahamasisha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha kujiunga na Chama Cha Wafanyakazi waandishi wa habari (JOWUTA), ambao yeye alichaguliwa hivi karibuni kuwa mwenyekiti wa JOWUTA Kitaifa.