Asasi ya smcct yavalia njuga kesi ya ubakaji wilayani ikungi mkoani singida

Mratibu
wa mradi wa  utetezi dhidi ya mila potofu na udhalilishaji wa
kijinsia kutoka Asasi isiyokuwa ya Kiselikari ya Save Mother and
Children of Central Tanzania (SMCCT) ya mkoani Singida, Evaline Lyimo
akizunguza na wanafuzi wa Shule ya Msingi Mapambano wakati wa kutathmini
mradi huo.
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
ASASI
isiyokuwa ya Kiselikari ya Save Morther and Children of Central
Tanzania (SMCCT) ya mkoani Singida imeanza kufuatilia kesi ya ubakwaji
wa mwanafunzi mwenye umri wa miaka nane wa darasa la pili katika Shule
ya Msingi Mapambano ambapo mtuhumiwa wake aliachiwa huru.
 
Hatua
ya asasi hiyo kufuatilia kesi hiyo ilitokana na kazi nzuri ya wajumbe
wa kamati ya ulinzi wa mama na mtoto na klabu ya wanafunzi ya kupinga
vitendo vya ukatili mashuleni iliyoundwa na asasi hiyo katika shule hiyo
kuibua tukio hilo ambapo mtuhumiwa alikamatwa na kuachiwa katika
mazingira ambayo hayaeleweki baada ya kupelekwa kituo cha polisi cha
Wilaya ya Ikungi huku wazazi wa mtoto huyo wakipigwa na bumbuwazi.
 
Akizungumza
katika kampeni maalumu ya siku sita ya kupinga vitendo hivyo na
tathmini ya mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu na udhalilishaji wa
kijinsia,  mratibu wa mradi huo kutoka asasi hiyo, Evaline Lyimo alisema
wamesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa huyo kuachiwa katika mazingira
ambayo hayaeleweki na kuacha zimanzi kwa familia ya mtoto huyo hasa mama
yake.
 

Wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mama na mtoto na klabu ya wanafunzi ya
kupinga ukatiki wa kijinsia tulioziunda ndio zilifanikisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo mtu mzima lakini tulishangaa baada ya kuona ameachiwa
huku mtoto akibaki na maumivu ya kubakwa” alisema Lyimo.
 
Alisema
tayari wamekwenda kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo
na mkurugenzi wa wilaya hiyo ambao wameahidi kulifuatilia suala hilo na
kulitolea majibu.
 
Mama
mzazi wa mtoto huyo akizungumza mbele ya viongozi wa asasi hiyo
waliokuwa katika kampeni hiyo ambayo imefadhiliwa na Shirika la
Foundation for Civil Society (FCS) inayolenga kutokomeza ukeketaji,
ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni  dhidi ya watoto alisema
anaviomba vyombo vya dola wilayani humo kuhakikisha anapata haki ya
suala hilo.
 
“Tumeachwa
njia panda hatujui tuanzie wapi na tunashangaa kumuona mtuhumiwa akiwa
nje na kila tukienda kuulizia kesi pale kituoni hatupati majibu ya
kueleweka na ni miezi miwili sasa imepita tangu mtoto wangu afanyiwe
kitendo hicho porini wakati akirudi nyumbani akitoka shule akiwa na
wenzake waliofanikiwa kukimbia wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa
akimfanyia unyama huo” alisema mama huyo ambaye jina lake tunalihifadhi.
 
Mratibu
wa mradi huo, Evaline Lyimo alisema katika kampeni hiyo shirika hilo
lilitembelea kata sita  na vijiji 18 pamoja na shule 25 zilizopo
wilayani  humo pamoja na kutathmini  mradi huo ambapo waliwatembelea
wahanga wa matukio ya ukatili kama kukeketwa, kubakwa,  kulawitiwa na  
wale ambao wamerudishwa shuleni baada ya kupatiwa elimu na shirika
hilo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *