Aaskofu ruwa’ichi aondolewa mashine



Hali
ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda
Ruwa’ichi, inaendelea kuimarika baada ya kutolewa katika mashine
iliyokuwa inamsadia kupumua na kuendelea kufanya mazoezi.





Askofu
Ruwa’ichi alifikishwa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (Moi)
akitokea Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu saa tano usiku
ambako alifanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo kwa saa tatu.



Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano Moi, Patrick Mvungi jana alisema  kuwa jopo la
wataalamu wa afya saba wanafuatilia hali ya Askofu Ruwa’ichi kila baada
ya saa moja.



“Kwa
sasa Askofu bado yuko ICU, lakini hatumii mashine ya kusaidia kupumua,
hii inaonyesha dalili nzuri na pia wataalamu wameanza kumfanyisha
mazoezi ya viungo akiwa kitandani, hivyo watu wasiwe na wasiwasi kwa
sababu afya yake inaendelea kuimarika siku hadi siku.



“Baada
ya mazoezi ya kitandani ataanza mazoezi ya kutembea na baada ya afya
yake kuimarika zaidi  atahamishiwa High Depend Word (HDU). Hii wodi ni
maalumu kwa ajili ya wagonjwa ambao afya zao zimeimarika,” alisema
Mvungi.