Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera
Wananchi mkoani Kagera wametakiwa kufuata taratibu za kuwapokea wageni
kutoka nchi jirani za Uganda Rwanda Burundi na Kenya na sio kuwa pokea
nakuwatunza kinyemera katika maeneo yao na kuwapa makazi bila kufuata
sheria za nchi.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya uhamiaji nchini Tanzaia Anna
Makakala wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mkuu
wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi itakayodu kwa siku tatu hapa
mkoani kagera ambapo kwasiku hizo tatu atazungukia wilaya zote za mkoa
wa kagera pamoja na kuzungukia mipaka ya mkoa wa kagera kwa upande wa
nchi jirani.
Makakala ameongeza kuwa Wageni kutoka nchi mbalimbali jirani waingie
nchini kwa kufuata taratibu maalumu na kuwa tahadharisha wananchi mkoani
hapa kuwa hatakaye bainika akimkaribisha mgeni pasipo kufuata sheria na
kanuni za nchi hatua kali za kisheria na hadhabu kali ya kifungo cha
miaka 20 au kutozwa faini ya milioni 20 zita chukuliwa dhidi yake.
Naye mkuu wa mkoa Kagera brigedia Generali Marco Gaguti amesema kuwa
mkoa wa Kagera hupo salama na hakuna wa amihaji haramu katika mkoa huu
ni kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na idara ya uhamiaji , na kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa kwa kushirikiana na wananchi.