Atupwa jela kwa kumuingizia uume mdomoni mtoto anyonye dar


Na Pamela Chilongola, Mwananchi 

 Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam imemuhukumu kifungo cha
miaka 20 jela mkazi wa Kimara Stop Over, Liziki Kessy baada ya kukutwa
na hatia ya kumwingiza uume wake kwenye haja kubwa na mdomoni mtoto wa
kiume mwenye umri wa miaka saba ili aunyonye.
Hukumu hiyo imesomwa leo Jumatatu Januari 20, 2020 na Hakimu Mkazi, Hudi
Hudi amesema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya
kupitia mashahidi watano wa upande wa mashtaka huku upande wa utetezi
ukiwa na mashahidi watatu akiwamo mshtakiwa mwenyewe.
Hudi amesema amezingatia shtaka hilo adhabu ya chini ni miaka 30 hivyo
mahakama hiyo imemuhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela miaka 20 .
Hudi amesema baada ya kupitia upande wa ushahidi wa mashtaka na ushahidi
upande wa utetezi mahakama hiyo imebaini mshtakiwa huyo alimfanyia
tendo la aibu kwa mtoto huyo.
Amesema kutokana na mtoto (muathirika) huyo kuieleza mahakama jinsi
mshtakiwa alivyomwita na kumpeleka kwenye jumba bovu huku akimvua
kaptura na kuanza kumuingizia uume wake kwenye haja kubwa na alipopiga
kelele ndipo mshtakiwa huyo aliuingiza uume kwenye mdomo wa mtoto huyo.
“Ushahidi wa muathirika umeungana na ushahidi aliyoutoa mama yake mzazi
pamoja na daktari wa hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ambaye alibaini
mtoto huyo alikuwa na michubuko kwa jinsi ilivyo kama kuna kitu kisicho
na ncha kimeingizwa sehemu ya haja kubwa,” amesema Hudi.
Via Mwananchi