Baba aliyekutwa akiwa uchi na mwanaye katikati ya maporomoko ya maji akamatwa morogoro

Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa
Polisi Wilbroad Mutafungwa akiwaonyesha wanahabari(hawapo pichani )
panga na msumeno alivyokutwa navyo, bwana Benson Benard (31) aliyekutwa
uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la
Mlimani Nguzo Camp.
Na Farida Saidy Morogoro
Jeshi La Polisi Mkoa wa Morogoro Benson Benard (31) aliyekutwa uchi wa
Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani
Nguzo Camp ndani ya manispaa hiyo na alipoamuliwa kuondoka eneo hilo
hatarishi akajirusha na kujizamisha kwenye Maji yaliyokuwa wakitiririka
kwa kasi kabla ya kushikiliwa na Polisi. 
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna msaidizi
mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa Askari wake walipokea taarifa
toka kwa raia mwema juu ya uwepo tukio hilo na baada ya kufika eneo la
tukio ambapo ni eneo la chanzo cha maji wakamkuta mtuhumiwa akiwa na
Mtoto wake , na katika hali ya kushangaza wote walikua uchi wa mnyama.
Aidha katika Eneo hilo la Tukio Askari Polisi walikuta Panga na Msumeno
ambapo pia kunadaiwa kumefanyika uharibifu wa mabomba ya maji, na sasa
mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo Mtoto amekabidhiwa kwa mama yake mzazi Mary Shao mkazi wa
Kihonda, ambae nae anasema muwewe alianza kubadilika kwa kuongea mambo
yasiyo eleweka na siku hiyo ya tukio aliaga anaenda kuogelea.