Bandari ya dar es salaam yapokea meli kubwa ya utalii iliyobeba watalii 600

Na Erick Msuya-MAELEZO

MALENGO
ya Tanzania kufikisha Watalii Milioni mbili kwa mwaka yameanza kutimia,
baada ya Watalii zaidi ya 600 kutoka mataifa mbalimbali duniani
kuwasili nchini kwa ajili ya ya kufanya utalii katika maeneo ya jiji la
Dar es Salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza
na waandishi wa habari jana  Alhamisi (Januari 9, 2020) Kaimu Meneja wa
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Joseph Sendwa alisema ujio wa
watalii hao utaongeza chachu ya Mapato na kuufanya uchumi wa nchi
kuinuka kupitia sekta ya Utalii.

“Ujio
wa Meli ya Watalii hapa nchini pamoja na Watalii kutembea katika Jiji
letu la Dar es Salaam, watatumia magari hivyo mzunguko wa mapato utakuwa
mkubwa ukiachilia mbali na mapato ya uhamiaji pindi wageni wanakiwasili
nchini” alisema Sendwa.

Sendwa
alisema TTB itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano
katika kukuza sekta ya utalii nchini ambapo imedhamiria kuweka
mazingira rafiki katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha kuwa gati
na. 1, 2, 4, 5 na 7 katika Bandari ya Dar es Salaam zinapokea idadi
kubwa ya watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Meli
hii ya watalii imetia nanga hapa kwenye Gati jipya kabisa, kwetu sisi
ni fahari na tunajivunia sana kwa hili, hivyo mataraijio yetu hapo
baadaye zije meli kama hizi mbili kwa pamoja ili kuongeza mapato katika
nchi yetu” alisema Sendwa.

Kwa
upande wake Mtalii, Whori Warabisako nchini Japani amesema kuja kwake
Tanzania ni fursa moja wapo ya yeye kujifunza utamaduni wa Matanzania na
kujione mazingira tulivu yaliyopo hapa nchini.

“Nafurahi
kuwepo hapa Tanzania, hii ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania na
nina amini kufika Tanzania nitajifunza mengi katika kuutembelea maneo ya
kitalii ya Tanzania” alisema whori Warabisako.

Watalii
hao kutoka Japani, Marekani, China, Tawain, Uingereza wamewasili leo
Alhamisi Januari 9, 2020 saa 12 asubuhi wakiwa katika Meli kubwa ya
Kisasa ya kampuni AZAMARA inayofanya safari zake Dunia nzima katika
kutangaza utalii wa majini.

Meli
hiyo ya AZAMARA itaondoka leo Alhamisi Januari 9, 2020 saa 4 usiku
kuelekea Zanzibar kwa lengo la kufanya utalii wa ndani katika maeneo ya
kihistoria ikiwemo Mji Kongwa,