Barabara zilizoharibiwa na mvua ukerewe kuanza kutengenezwa


Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoana serikali za Mitaa Josephat
Kandege akiwa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe wakati wa Ziara yake ya
kikazi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Maendelea pamoja na
barabara zinazotengenezwa na Tarura.


Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoana serikali za Mitaa Josephat
Kandege akiwa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe wakati wa Ziara yake ya
kikazi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Maendelea pamoja na
barabara zinazotengenezwa na Tarura.

Na Geofrey A. Kazaula – UKEREWE
Naibu
waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI
Mhe, Josephat Kandege ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na
Mijini TARURA kufanya ukarabati kwa barabara zilizoharibiwa na mvua
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.



Ameyasema
hayo alipotembelea barabara hizo ili kujionea hali halisi ikiwa ni
mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
Mkoani Mwanza.

‘‘TARURA
mnafanya kazi nzuri ila nitoe wito kuwa pale mnapo endelea na ujenzi wa
barabara hizi mjitahidi kuangalia maeneo korofi yaliyoharibiwa sana ndo
mkaanze nayo ili wananchi hawa wapate huduma’’, amesema kiongozi huyo.

Kwa
upande wake Mkurugenzi wa barabara za Vijijini kutoka TARURA Mhandisi
Abdul Digaga amesema kuwa tayari kuna fedha kiasi cha Sh 50 Millioni
zilizoletwa Ukerewe kwaajili ya kufanya matengenezo ya barabara hasa kwa
maeneo yaliyoharibiwa na mvua ambapo Meneja wa TARURA Katika
Halmashauri ya Ukerewe Mhandisi Reuben Muyungi amekiri kupokea fedha
hizo na kwamba Mkandarasi tayari amepatikana na kazi itaanza wiki ijayo.

Naye
Mbunge wa Ukerewe Mhe, Joseph Mkudi amesema kuwa kazi inayofanwa na
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini – TARURA ni kubwa na kusema
kuwa kuna haja ya Serikali kuongeza bajeti ya Wakala huo ili uweze
kutekeleza majukumu yake kwa urahisi kwani kazi inayofanyika inaonekana
licha ya ufinyu wa bajeti.

‘‘Mimi
kama mbunge nitaendelea kujenga hoja kwa Serikali ili iongeze bajeti ya
TARURA barabara zetu ziweze kutengenezwa kwa urahisi na kuwapatia
wananchi wetu huduma’’ amesema Mkudi.

Mmoja
wa wananchi Katika Kata ya Ukerewe Ndg,Nesphory Kangi amesema kuwa
TARURA inasaidia sana kuwajengea barabara na miundombinu miingine na na
kwamba kuna upungufu wa barabara za lami ambapo ameomba Serikali
iwaongezee barabara hizo.

Miradi
mingine iliyokaguliwa na Mhe, Kandege ni pamoja na Kituo cha Afya cha
Busya -Ukara, Vikundi vya akina mama vinavyokopeshwa na Halmashauri
kupitia mgawanyo wa asilimia kumi ya mapato ya ndani pamoja Ujenzi wa
Vyumba vya madarasa vine na Ofisi moja ya Walimu Katika shule ya Msingi
Murunsuli ambapo pia ameweka jiwe la Msingi.