Baraza la kinamama wa kifugaji pwc lakabidhi msaada wa vifaa vya mapambano dhidi ya covid 19

table align=”center” cellpadding=”0″ cellspacing=”0″ class=”tr-caption-container” style=”margin-left: auto; margin-right: auto; text-align: center;”>

Mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Kimanta akipokea Ndoo Mia mbili na vitakasa mikono lita 140 kutoka kwa kiongozi wa baraza la kinamama wa kifugaji kwenye halfa iliyofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo leo wilayani humo picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Stephen Ulaya aliposhiriki halfa ya kukabidhiwa vifaa vya mapambano ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 leo wilayani humo picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Sehemu ya ndoo Mia mbili na sabuni Lita  147 na vitakasa mikono kama vivyokutwa na kamera ya matukio wilayani Monduli picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Makabidhiano yakiendelea kwenye eneo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Monduli leo leo wilayani Monduli

Picha ni vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 vilivyotolewa na baraza la kinamama wa kifugaji leo wilayani Monduli picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Monduli  Iddi Hassani Kimanta ameitaka jamii kuendelea kuchukuwa hatua mbali mbali za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Corona ikiwemo elimu zinazotolewa na wataalamu wa sekta ya Afya.

Aidha ameiasa jamii kuacha kuendelea na mikusanyiko isiyo ya lazima ambayo imekatazwa na wataalamu na ile ya lazima wachukue hatua ya Uvaaji wa barakoa kuendelea kudhibiti Ugonjwa huo

 Kimanta Ameyasema hayo wakati akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Stephen Ulaya wakipokea msaada wa Ndoo 200,Barakoa 500 na Sabuni lita 140 kutoka  Baraza la akina mama wa kifugaji l(Pastrol Women Council) huu -PWC.

Msaada huo umetolewa kwa  Wilaya hiyo  kusaidia kupambana na Ugonjwa wa Covid_19 unasababishwa na virusi vya Corona wilayani humo.

Akipokea Msaada huo Mkuu wa wilaya  amelishukuru sana Baraza kwa Msaada huo muhimu kwa Wilaya kwa kuwa bado inamahitaji ya vifaa katika kukabiliana na janga hilo la Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Ndg.Stephen Ulaya amesema pamoja na  kutoa shukrani ameomba wadau wengine waige mfano wa Baraza hili la akina mama
  Wakifugaji.

MONDULI BILA CORONA INAWEZEKANA