Baraza la madiwa halmashauri ya wilaya ya shinyanga lamtaka mkurugenzi kuwa na takwimu ya wawekezaji


Na Mapuli Kitina Misalaba

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga limemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa na takwimu sahihi
ya wawekezaji ili kunufaika na miradi ya wajibu kwa jamii CSR  hasa katika zoezi la ukusanyaji wa mapato.

Maelekezo hayo yametolewa leo Machi 6,2024 na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje kwenye
mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupokea na kujadili taarifa
za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka
kwenye kata mbalimbali katika kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha
20232024.

Mhe. Mboje ameyasema hayo baada ya Madiwani wa
Halmashauri hiyo kuhoji kwa Mkurugenzi hali ya ukusanyaji wa mapato kwa
wawekezaji katika migodi hasa Mwakitolyo pamoja na Mwenge ambao kwenye taarifa
ya Mkurugenzi hawakubainishwa kuwa sehemu ya wajibu kwa jamii CSR.

“Wajumbe
hawakuweza kuridhishwa na orodha kwahiyo tunachokihitaji ni orodha ya wale
wawekezaji  na namna gani Halmashauri
inanufaika orodha ya wawekezaji ambao Baraza liliwahitaji hawapo lakini pia ule
unufaika kwa sasa ni kidogo tunataka wawekezaji ambao Baraza liliwahitaji
wawekwe ili tulinganishe idadi ya wawekezaji waliopo na kile tunachokipata
vinawiana”.

“Mtendaji
wa kata alikuja nikampa orodha ya makampuni yote yaliyowekeza kwenye kata yangu
ya Mwakitolyo sasa leo hii siyaoni kwenye maadhimio kwanza ni zaidi ya
makampuni manne mimi najisifu kwamba kata yangu ni kata ya wawekezaji lakini
ninapokuja kwenye Baraza siyaoni sasa haya makampuni yanapita pitaje”.

Mpaka sasa Halmashauri hiyo imefikia asilimia
takribani 40 ya ukusanyaji wa mapato kwa Mwaka wa Fedha 20232024 ambapo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje ametumia
nafasi hiyo  kumuelekeza Mkurugenzi na
wataalam wake kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ikiwa ni pamoja na kuongeza
vyambo vya mapato ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

“Wewe
unajua kabisa kuwa mapato hamko vizuri lakini Madiwani wanaoishi kule kwenye
hizo kata wamekuonyesha wawekezaji lakini haujatoa ushirikiano tunataka kujua
mpaka sasa umechukua hatua gani kama umewaagiza wataalam wako kwenda kuchukua
orodha na wameshaichukua Diwani ametoa ushahidi kuna shida gani mpaka sasa
orodha ya makampuni bado haijakufikia wakati watendaji walichukua orodha mi
nadhani kuna udhaufu mkubwa kwenye ukusanyaji wa mapato inawezekana siyo wewe
Mkurugenzi ila wale wataalam wako wanaokusaidia kwahiyo unatakiwa uchukue
mawazo yetu kwamba sisi tumeona kunashida unatakiwa kuchukua hatua kwa
wahusika, mimi naagiza tu kwamba atuletee hatua alizochukua kwa wahusika ambao
wamechukua orodha Mwakitolyo mpaka sasa hawajaiwasilisha kwake”.
amesema
Mwenyekiti Mboje

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesisitiza
kuwa ni vema Halmashauri hiyo kuweka mikakati ya pamoja kwa kushirikiana na
Madiwani kuhakikisha  zoezi la ukusanyaji
mapato linafikia malengo ambapo ameagiza siku ya Ijumaa wiki hii kupata orodha
ya wawekezaji wote katika Halmashauri hiyo ili hatua zaidi zianze kuchukuliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Shinyanga vijijini Mhe. Edward Ngelela naye amehimiza kila kata kuhakikisha inashiriki
kikamilifu katika zoezi la ukusanyaji wa mapato.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Kisena Mabuba ameahidi kushughulikia maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa kwa
lengo la kuleta matokeo chanya ambapo amesema kuwa tayari amewaelekeza
watendaji kutoka kwenye kata, kuhakikisha wanahudhuria kwenye vikao vya Baraza
la Madiwani ili kuepusha changamoto inayojitokeza hasa katika ukusanyaji wa
mapato.

Aidha Madiwani kutoka  Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Shinyanga
wamewasilisha taarifa mbalimbali za kata zao huku  wakitaja changamoto mbalimbali ikiwemo  ya ubovu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo
kwenye kata zao pamoja na uhitaji wa Zahanati kwenye vijiji.

Pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Mhe. Ngassa Mboje amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuanza mchakato wa
kutoa Fedha kwa ajili ya kumalizia jingo la kituo cha Polisi kata ya
Iselamagazi ambayo ni ahadi ya Halmashauri hiyo kutoa Milioni kumi kwa ajili ya
kumalizia boma lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

Ametoa agizo hilo baada ya diwani wa kata ya
Iselemagazi kuhoji ukamilishwaji wa boma lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

“Sisi
tunajengo hapa la kituo cha Polisi ambalo lilijengwa kwa nguvu za wananchi Halmashauri
iliahidi kutoa Milioni kumi na dhani ni Miaka sita au Mitano iliyopita na
tunajua umuhimu wa kituo cha Polisi hapa ni makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga hatuna ulinzi sahihi tunajengo kubwa mno tulishakamilisha kwa
maana ya boma lakini sasa niombe ile ahadi ya Milioni kumi tupate ili jingo hilo
likamilike”.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Mhe. Ngassa Mboje akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo leo kwenye
mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupokea na kujadili taarifa
za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka
kwenye kata mbalimbali katika kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha
20232024.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Mhe. Ngassa Mboje akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo leo kwenye
mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupokea na kujadili taarifa
za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka
kwenye kata mbalimbali katika kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha
20232024.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza
kwenye Baraza hilo leo Jumatano Machi 6,2024.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya
Shinyanga vijijini  Mhe. Edward Ngelela akizungumza
kwenye Baraza hilo leo Jumatano Machi 6,2024.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Kisena Mabuba akiahidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo.

Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga
kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka kwenye kata mbalimbali katika
kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 20232024 ukiendelea leo Jumatano
Machi 6,2024.

Diwani kata ya Ilola Mhe. Amosy Mshandete akizungumza kwenye Baraza hilo.

Diwani wa kata ya Salawe Mhe.Joseph Buyugu akizungumza kwenye Baraza hilo.

Diwani wa kata ya Mwakitolyo Mhe. Masalu Nyese akizungumza kwenye Baraza hilo.


Diwani wa kata ya Iselamagazi Mhe. Isack Sengelema akizungumza kwenye Baraza hilo.