Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya kishapu limejadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya halmashauri hiyo na tarura kwa mwaka wa fedha 2024/2025

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza kwenye Baraza hilo leo Februari 20,2024.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu limejadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya Halmashauri hiyo
ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 yenye jumla ya shilingi Bilioni 40 Milioni 821 na
3372.

Tamko hilo limetolewa leo
Februari 20,2024 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William
Jijimya baada ya Madiwani kurithia kwa pamoja mapendekezo hayo.

Baraza hilo limepitisha mapendekezo ya
bajeti  huku wakisisitizwa watendaji wa
Halmashauri hiyo kuendelea kushirikiana na viongozi wengine wakiwemo Madiwani hasa
katika suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.

“Wote
kwa pamoja baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu tumejadili na
kupitisha mapendekezo ya bajeti ya Halmashauri 
ya Mwaka 2024/2025 yenye jumla ya shilingi Bilioni 40 Milioni 821 elfu
3372”.

“Kupitisha
bajeti siyo suala tu la makaratasi twendeni tukashikane mashati kwa ajili ya
ukusanyaji wa mapato tusiruhusu chochote kitoke kwenye Halmashauri yetu bila
kutoa ushuru tunaomba mkurugenzi kupitia wataalam wako tuonyesheni ushirikiano
watendaji mtusikilize na siyo tu kutusikiliza nendeni mkatende kama ambavyo
tumeshauri ili kuwaweka sawa wananchi wetu”.
amesema
Mwenyekiti Mhe. Jijimya

Pia Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu limepitisha mpango na mapendekezo ya bajeti ya matengenezo ya Barabara
kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ambayo itatekelezwa na wakala wa Barabara za
vijijini na mijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Kishapu.

Awali akisoma taarifa ya mapendekezo hayo
kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Hussein Shaweji amesema zaidi
ya Bilioni mbili zitatumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo  matengenezo ya barabara kwa lengo la
kuboresha miundombinu ya Barabara katika Wilaya ya Kishapu.

Wakati huo huo baadhi ya Madiwani wa kata
mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wameitaka TARURA kutekeleza kwa
vitendo bajeti hiyo ikiwa ni pamoja na kuyafikia maeneo korofi hasa kipindi
hiki cha msimu wa mvua ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu Emmanuel Jonhson ameahidi kusimamia mpango huo wa bajeti uliopendekezwa
Mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo suala la
ukusanyaji wa mapato ya ndani.

“Niwashukuru
kwa kujadili na kupitisha bajeti zetu zote mbili bajeti ya TARURA na bajeti ya
Halmashauri niwaahidi kwamba yale mapendekezo tuliyokubaliana tutayasimamia,
sisi mmetuachia kazi tunajukumu la kuhakikisha tunakusanya mapato ili kile
kilichoidhinishwa kikatekelezwe kwa ukamilifu”.
amesema
Mkurugenzi Jonhson.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mhe. Joseph Mkude amesisitiza viongozi wa serikali na wataalam mbalimbali
kuendelea kushirikiana na Madiwani katika kubaini na kutatua changamoto za
wananchi.

“Kinachotakiwa
ni mawasiliano na kusikilizana na katika hili nisisitize watumishi wenzagu wote
tukianza na mimi mwenyewe, Mkurugenzi, watendaji wa mamlaka za Serikali za
mitaa lakini pia wezetu TARURA, RUWASA na wengine jamani tuwasikilize sana
waheshimiwa Madiwani halafu tuwatimizie kwa sababu ndiyo hayo yanayotoka kwa
wananchi”.
amesema DC Mkude

Aidha Baraza hilo la Halmashauri ya Wilaya
ya Kishapu pamoja na viongozi wengine wa serikali akiwemo mkuu wa Wilaya ya
Kishapu Mhe. Joseph Mkude wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua kero za wananchi kupitia Fedha
za miradi mbalimbali huku wakimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe.
Boniphace Butondo kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza kwenye Baraza hilo leo Februari 20,2024.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza kwenye Baraza hilo leo Februari 20,2024.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Jonhson akizungumza kwenye Baraza hilo leo Februari 20,2024.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza kwenye Baraza hilo leo Februari 20,2024.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu likiendelea leo Jumanne Februari 20,2024. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *