Barua ya rais magufuli yatua bungeni dodoma

Spika
wa Bunge Job Ndugai amesema Rais Magufuli amepokea azimio la pongezi
lililofikiwa na Bunge kwenye kikao cha 17, kufuatia mafanikio na mageuzi
kwenye utendaji kazi wa Serikali na pia ameandika barua ya kulishukuru
Bunge kwa kutambua mchango wake.

Barua
hiyo ya Rais imesomwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 18 na Spika wa
Bunge la Tanzania Job Ndugai  ambapo amesema Rais Magufuli analishukuru
Bunge kwa kutambua mchango wake wa kuliletea maendeleo Taifa.

“Niendelee
kuwaasa Wabunge na watanzania kwa ujumla tuendelee kuipambania nchi
yetu, ili tuweze kufikia maendeleo yenye uchumi wa kati” amesema Spika
Ndugai wakati akisoma barua ya Rais Magufuli.