Bashe:serikali imeamua kuheshimu na kuweka kipaumbele sekta ya kilimo

Na.Faustine Galafoni,Dodoma.

NAIBU
Waziri wa Kilimo,Husein Bashe amesema Serikali imeamua kuheshimu na
kutoa kipaumbele mazao ya kilimo kama sekta zingine zinavyothaminiwa kwa
kujenga miundo mbinu rafiki kwa mkulima hususani pembejeo bora.


Kauli
hiyo ameitoa wakati alipokuwa kwenye mkutano wa kitaifa wa wakulima
wadogo Tanzania uliofanyika jijini Dodoma kujadili changamoto
wanazokumbana nazo ulioandaliwa na Shirika la ANSAF.

Waziri
Bashe amesema kuwa sekta ya kilimo imekuwa msaada katika kuinua uchumi
wa nchi kutokana na kaya ,jamii kwa ujumla kutumia malighafi nyingi
zinazotokana na kilimo mbali na changamoto zinazowakabili wakulima .

Amebainisha
tarari serikali imeweka mikakati ya kuboresha miundo mbinu kwa wakulima
wadogo katika suala zima la kuongeza maafisa ugani vijijini huku
wakishirikana na maafsa watendaji kutembelea wakulima,pembejeo zilizo
bora na bei rahisi,upatikanaji wa mbegu nzuri,sheria ya kulinda
wakulima,kuwapatia Bima ya mazao ,pamoja na kuongea na taasisi za
kifedha kupata mikopo yenye riba nafuu jambo ambalo litasaidia kuleta
maendeleo.

“Kama
Wizara itaendelea kutangaza  na kuhamasisha wakulima wadogo kuboresha
miundo mbinu ili kuwe na kilimo chenye tija  kwani wamekuwa wachangiaji
wazuri uchumi wa nchi na jamii imategemea chakula kutoka kwa wakulima
wadogo”alisema Waziri Bashe.

Hata
hivyo amepiga marufuku kwa viongozi wa Ushirika ambao sio wakulima
kuongoza wakulima kutokana na malalamiko yanayotolewa ambapo wao kazi
kubwa ni kujinufaisha badala ya kuwasaidia wakulima hao.
“Kuanzia
leo kiongozi ambaye sio mkulima hapaswi kuongoza wakulima haiwezekani
wewe sio dhehebu ya kiislamu halafu eti uwaongoze waislamu”amesema.

Mbali
na hayo amesema wizara imeanzisha Dawati la masoko ambalo
litashughulikia wakulima ambao ufanyiwa ukiritimba na TBS huku akisema
kutakuwa na huduma bure ya mawasiliano ambayo itawala fursa wakulima
kupiga simu kueleza changamoto zao na kutatuliwa hapo hapo.

Nae
mwenyekiti kamati ya Bunge kilimo,mifugo na maji Mahamoud Mgimwa
amesema wabunge wako tayari kuendelea kuwatetea wakulima ili serikali
iweze kutatua changamoto zao lengo ni kufikia asilimia kumi .

Kwa
upande wake  Mwenyekiti jukwaa la wakulima wadogo wanawake ,Janeth
Nyamayahasi amesema wanakumbana na changamoto ya upungufu wa maafisa
ugani vijijini kwenye sekta ya mifugo,kilimo na uvuvi na kwamba baadhi
ya wataalamu hao hawatoi ushirikiano na mara utoa ushauri mbovu
unaopelekea mazao yao kuharibika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *