Basi la freys coach laungua moto likitoka shinyanga kwenda tanga


Na Josephine Charles – Malunde 1 blog

Basi la Freys Coach lenye namba za usajili T119BDY Gari la Freys Coach linalofanya safari zake kutoka Shinyanga kwenda Tanga limeungua moto katika eneo la Mhizi Usanda Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga barabara ya Tabora – Shinyanga.

Tukio hilo limetokea leo Ijumaa Oktoba 18,2019 majira ya saa 12 na nusu baada ya kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio wanasema basi hilo limeungua matairi mawili ya nyuma upande wa kulia na kwamba hakuna madhara yaliyojitokeza kwa abiria.

Inaelezwa kuwa abiria walishuka na kuanza zoezi la kuzima moto huo kwa maji na mchanga na muda mfupi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio na kufanikisha kuzima moto huo.

“Tumezima kwa maji na mchanga,zimamoto nao wamefika,gari limezima,hakuna uharibifu wa mali za abiria wala majeruhi,gari halijateketea lote,abiria tumefanya juhudi za kuzima moto,sasa tunasubiri magari mengine kutoka Mwanza ili tuendelee na safari yetu”,wamesema abiria wakizungumza na Malunde 1 blog.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadae.

Muonekano wa basi la Freys Coach baada ya kuungua leo. Picha zote na Josephine Charles – Malunde 1 blog